Na. Theresia Francis, DODOMA
Mratibu
wa Sensa ya watu na makazi wa Wilaya ya Dodoma, Calister Makacha amewashauri wakazi
wa wilaya hiyo kushiriki zoezi la Sensa ya watu na makazi kwa kujitokeza
kuhesabiwa tarehe 23/08/2022 kwa maendeleo ya taifa.
Kauli
hiyo aliitoa wakati akiongea na waandishi wa habari katika ukumbi wa mikutano
wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma.
“Sensa
ni zoezi zima lakukusanya taarifa, kuzichakata, kuzichambua na kutoa ripoti
maalumu kwaajili ya kukusanya takwimu za kidemografia, kiuchumi, mazingira
lakini takwimu zote za watu pamoja na makazi yao” alisema Makacha.
Aidha,
alielezea umuhimu wazoezi hili kwa serikali ya Tanzania kuwa zoezi hilo
litasaidia kupata takwimu rasmi ambazo zitaisaidia katika kupanga mipango ya
maendeleo ya taifa.
Sambamba
na hilo, Machaka alielezea utaratibu wa Sensa hiyo ya sita toka zoezi la Sensa lianze mwaka 1978
itakayofanyika mwezi Agosti. Sensa hiyo itafanyika kwa njia ya kielektroniki kwa
kutumia vishikwambi. Hivyo, makarani watakaoendesha zoezi hilo hawatakuwa na
madodoso ya makaratasi kama ilivyokua miaka ya nyuma.
“Maswali
yote yataingizwa kwenye vishikwambi na watahoji kuanzia mwanzo hadi mwisho kwa
dodoso kuu, dodoso la majengo na dodoso la makazi” aliongeza Makacha.
Sensa
ya watu na makazi kwa mwaka 2022 inaongozwa na kaulimbiu isemayo “Sensa kwa
maendeleo, jiandae kuhesabiwa”.
MWISHO
Comments
Post a Comment