DODOMA.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira
Dkt. Seleman Jafo amesema eneo la msitu
la Iyumbu Park likitumika vizuri linaweza kuwa chanzo cha utalii na kuvutia watu
wanao kuja Dodoma ili waweze kujionea utalii uliomo katika eneo hilo.
Eneo hilo lina zaidi ya hekari 3000 limekuwa eneo maalum lililo
tengwa kwaajili ya kupanda miti.
Dkt. Jafo ametoa kauli hiyo leo jijini Dodoma wakati
akizindua rasmi Wiki ya Mazingira , amesema katika baadhi ya miji wamekuwa
wakiingiza fedha nyingi kupitia maeneo maalum ya misitu yaliyo hifadhiwa ambayo yamo katikati ya jiji kwa
watalii wanao kwenda kutembelea maeneo hayo.
‘’Na hapa Dodoma tumetenga eneo hili. Na Dodoma ni makao Makuu ya nchi yetu . Sasa nina amini miti hii tukiipanda na kuitunza itakuwa ni
jambo jema sana . Ndugu zangu kama mnavyo fahamu mabadiliko ya tabianchi
yamekuwa na changamoto kubwa duniani . Hali ya leo hii mnaona suala zima la
ukame maeneo mbalimbali mvua zinazo nyesha hazitoshelezi yote ni changamoto ya
ukame.’’ amesema Dkt. Jafo
Kwa upande wa Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Antony Mtaka ameagiza
kwa kila mtu mwenye kiwanja Dodoma
kuhakikisha anapanda miti ya matunda na
miti ya kuvuli ili kuandoa changamoto za utapiamlo na udumavu unao sababisha
kutozingatia lishe bora.
‘’Hata ukiangalia katika maeneo mengi tuliyo pita hakuna miti
ya matunda ,huoni michungwa,huoni miembe . kwa hiyo tunajaribu kuhamasisha kuwa
mabalozi wazuri wa upandaji wa miti katika familia .‘’ amehimiza Mtaka
Naye, Mkurugenzi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na
Mazingira Dkt. Andrew Komba amesema miti 441 imepandwa katika eneo hilo huku lengo
likiwa ni kupanda miti 3000.
‘’ Mwaka jana tulipanda miti mahali hapa tulipanda miti
takribani 241. Kazi tunayo fanya ni muendelezo wa kazi tuliyo kuwa tukiifanya na
tutaendelea kuifaanya . Lengo ni kuhakisha kwamba eneo lote hili la Iyumbu Park
linaenda kupandwa miti.’’
Wiki ya Mazingira imezinduliwa ikiwa ni sehemu ya Maadhimisho
ya Siku Mazingira Duniani yanayo tarajiwa kufanyika Juni 5,2022.
Mwisho.
Comments
Post a Comment