Na Shaban Ally, DODOMA
Mkuu
wa Wilaya ya Dodoma, Jabir Shekimweri awashauri watumishi wa umma kutendea haki
ongezeko la asilimia 23.3 ya mishahara yao iliyotolewa na Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania kwa kufanya kazi kwa uadilifu na ubunifu kwa kuzingatia
haki na maslahi mapana ya nchi.
Jabir Shekimweri |
Ushauri
huo aliutoa leo katika hafla fupi ya kumshukuru na kumpongeza Rais wa Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania kwa kuboresha maslahi ya watumishi katika ukumbi wa
mikutano wa PSSSF jijini hapa.
“Kutokana
na juhudi na kazi kubwa inayoendelea kufanywa na Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, sisi kama watumishi wa umma
tusishangilie ongezeko la mishahara bali tunapaswa kutendea haki mishahara
iliyoongezwa na Mheshimiwa Rais" alisema Shekimweri.
Mkuu
wa wilaya huyo alitoa rai kwa watumishi wa umma kuboresha maisha yao katika
kipindi hiki cha ongezeko la mishahara. Alisema kuwa watumishi wengi wa umma
wamekua wakiishi maisha ya taabu kutokana na kutokuwepo na matumizi mazuri ya
mishahara yao.
Aidha,
alimpongeza Rais, Samia Suluhu Hassan kwa kutunukiwa tuzo ya uendelezaji wa
miundombinu na Benki ya Maendeleo ya Afrika pamoja na kuwa miongoni mwa
viongozi 100 bora wenye ushawishi duniani walioorodheshwa kwenye jarida la
kimataifa la Forbes.
MWISHO
Comments
Post a Comment