WAZIRI CHANA AIPONGEZA MALIASILI SPORTS CLUB

 

Waziri wa Maliasili na Utalii, Balozi Dkt. Pindi Chana ameipongeza timu ya mpira wa Miguu ya Wizara ya Maliasili na Utalii kwa kuwa mshindi wa kwanza kwenye michezo ya Mei Mosi.

 

Waziri wa Maliasili na Utalii, Balozi Dkt. Pindi Chana (kushoto)

Mhe. Chana licha ya kuipongeza timu hiyo amewapongeza wachezaji na kuwataka watumie ushindi huo kama chachu ya kuongeza juhudi na ufanisi kazini utakao endana na kasi ya matokeo chanya ya Filamu ya The Royal Tour iliyozinduliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan Jijini Arusha.

 

Kwa upande wake Katibu wa Michezo wa Wizara ya Maliasili na Utalii, (Maliasili Sports Club) Bi. Labi Masalu amemshukuru Mhe. Waziri Pindi Chana kwa kuiunga mkono Club hiyo ya michezo na akiahidi kutekeleza agizo alilowapa. 

 

Michezo ya Mei Mosi hufanyika kila mwaka kwa kujumuisha wafanyakazi wote wa Serikali na Sekta binafsi ambapo kwa mwaka huu yamefanyika Jijini Dodoma na timu ya miguu ya Wizara ya Maliasili na Utalii kuibuka na ushindi.

 

Comments

Dodoma News
Mwanza City, Mwanza, Tanzania
Dennis G. Harrison, mmiliki mwenza wa Mtandao wa Dodoma News Blog, alizaliwa mkoani Morogoro zaidi ya miaka 40 iliyopita. Dennis ana Taaluma ya Uandishi wa Habari (Proffessional Journalism) kutoka Chuo Kikuu cha Mtakatifu Augustine (SAUT). Mwaka 2009 alimaliza Shahada ya Uzamili katika Mawasiliano ya Umma, ikijikita katika Menejimenti ya Uhusiano kwa Umma na Matangazo katika chuo cha SAUT. Mwaka 2002, Dennis aliajiriwa katika Shirika la Posta Tanzania, Ofisi kuu ya Mwanza. Mwaka 2009 aliajiriwa katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Iringa kwa nafasi ya Afisa Habari. Akiwa katika ofisi hiyo alifanya kazi kwa juhudu na maarifa na kufanikiwa kuchaguliwa na wafanyakazi wote kuwa mfanya kazi bora. Kufuatia juhudi na utendaji kazi wake, alipanda hadi nafasi ya Afisa Habari Mwandamizi.