Na
MJJWM- Dar Es Salaam
Waziri
wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Dkt. Dorothy Gwajima
amewasihi wasiachana kujitokeza kwa wingi kujifunza na kubobea kwenye ujuzi na
maarifa ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) kwani kwa sasa tafiti
zinaonesha asilimia 90 ya ajira kwa kipindi kijacho zitahiji ujuzi wa TEHAMA.
Dkt.
Gwajima ameyasema hayo leo Aprili 28, 2022 jijiini Dar Es Salaam wakati
akizindua wa pili Program ya Kuhamasisha Wasichana Barani Afrika kushiriki
katika TEHAMA, Mpango ambao utawawezesha wasichana walio wengi kuwa na ushiriki
mpana kwenye masuala ya teknolojia.
Dkt.
Gwajima amefafanua kuwa, kwa sasa Serikali ya Tanzania, imeridhia kutekeleza
mikataba ya kimataifa na ya kikanda ikiwepo mkataba wa kutokomeza ubaguzi wa
aina zote wa mwaka 1978, Azimio la Beijin la 1996, Mkataba wa Kimataifa wa Haki
za Mtoto wa 1989, Mpango wa Maendeleo Endelevu wa 2030, Ajenda ya Afrika
tunayoitaka ya mwaka 2063 na Mkataba wa Afrika wa Haki ya Mtoto wa 1989.
“Mikataba
hii na mingine ina lengo la kuhakikisha kunakuwa na usawa wa kijinsia hivyo
kama jamii ya watanzania, tunayokila sababu yakuweza kuyafikia malengo hayo
kwakuzingatia muda uliowekwa” alisema Dkt. Gwajima
Akizungumza
kwenye uzindunzi huo Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto wa
Zanzibar, Mhe. Riziki Pembe Juma, amesema kama ilivyo kwa Tanzania Bara, kwa
upande wa Zanzibar wamekuwa wakitoa kipaumbele kwa watoto wa kike kupitia
Programu ya Fawe na Femu lakini pia kupitia Chuo Kikuu cha Zanzibar na Chuo
kikuu cha Karume.
“Kama
ilivyo kwa Tanzania Bara, tunachofanya kwa sasa nikuwawezesha wanawake wa
vijijini kwenye Programu mbalimbali za Kisayansi ikiwepo ile ya kuwawezesha
kutengeneza taa za umeme wa jua, hivyo mbali ya kujikita kwa kuangalia waliopo
vyuoni vile vile kipaumbele tumekiweka pia kwa walio nje ya Vyuo" alisema
Mhe. Riziki
Kwa
upande wao mabinti Thereza Joseph wa Tanzania na Fatou Ndiaye kutoka Senegal
waliokuwa wakisomea fani ya TEHAMA, wamepongeza juhudi zinazochululiwa kwa sasa
katika nchi za kiafrika katika kuwawezesha watoto wa kike kupata elimu na ujuzi
mbalimbali.
“Mwanzoni
sisi wakati tupo Sekondari tunajifunza kusuka mifumo wengi tulikuwa hatujua
hatma yetu, lakini kutokana na msukumo huu unaowekwa na Serikali zetu tunaimani
kabisa, utamwezesha Msichana kufikia malengo yake, maana kama unavyofahamu,
jamii nyingi za kiafrika zilikuwa hazitoa kipaumbele kwa watoto wa kike kwenye
suala elimu, lakini kwa muamko huu tunaiona kesho yetu” alisema Thereza kutoka
Tanzania.
Akizungumza
kwenye Uzinduzi huo, Lilian Mwamdanga Mkuu wa Idara ya uwezeshaji wa wanawake
kiuchumi, amesema Program hiyo itakwenda kufanyika katika mwaka wa fedha
2022/23, ambapo jumla ya Nchi 11 zitashiriki kwenye mpango huo zikiwepo
Tanzania, Burundi, Mozambique, Niger, Mali, Kenya, Rwanda, DR Congo, Senegal,
Uganda na Afrika Kusini
MWISHO
.jpg)
Comments
Post a Comment