NAPE AWATAKA WAFANYAKAZI WIZARA YA HABARI KUZINGATIA MISINGI YA SHERIA.

 


Na Rhoda Simba, Dodoma.

 

WAZIRI wa Habari,  Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Nape Nnauye amewataka wafanyakazi  wa Wizara hiyo kufanya kazi kwa  bidii na weledi kwa kuzingatia misingi ya sheria, haki na ustawi kwa wateja wanaowahudumia.

 

Waziri Nape ameyasema hayo leo Aprili 30 jijini hapa  katika kikao cha wafanyakazi wa Serikali na Afya TUGHE  ambapo amesema  baadhi ya watumishi wa umma  wanafanya kazi kwa mazoea hali  inayoathiri uwajibikaji wa pamoja katika utoaji wa huduma  kwa  wananchi.

 

“Ninawaomba watumishi tuache kufanya kazi kwa mazoea, ondokeni katika kufanya kazi kwa analojia na badala yake tuhakikishe tunafanya kazi zitakazoacha alama"amesema Nape

 

“Kila binadamu ana vipawa ambavyo Mungu amempa, ni matumaini yangu kwamba haya tunayoanza kuyajenga sisi wafanyakazi tutayatumia vizuri, tutimize wajibu wetu na kila mmoja kwenye eneo lake aone umuhimu wa kuwa hapo alipo.”ameongeza Nape

 

Pamoja na hayo, amesema Wizara hiyo inasimamia miradi mikubwa kadhaa ambayo itabadilisha na ni vizuri kama Wizara wakawa na uelewa wa pamoja wa miradi  kupitia semina mbalimbali.

 

“Dunia inabadilika na sisi tuko kwenye Wizara ambayo inajenga kesho, mabadiliko ya sayansi na teknolojia yanabadilisha namna ambavyo tunapaswa kufanya kazi hivyo ni muhimu kila mmoja kwenye eneo lake kuhakikisha anafkiria zaidi ya ‘google’ ili kuonesha umuhimu wa kuwa katika nafasi hiyo”amesema

 

Naye ,Katibu Mkuu Wizara ya  Habari  mawasiliano  na Teknolojia ya  Habari Dkt Jimmy Yonazi ameahidi kuboresha  mazingira  ya kazi  kwa wafanyakazi.

 

“Jambo la kufanya kazi kwa furaha kwangu mimi ni kipaumbele, wajibu na nia, kila mmoja anatakiwa kufanya kazi kwa uhuru na kuruhusiwa kufikiri kwa sababu kufikiri kwa uhuru kunaleta ubunifu,

 

“Katika ulimwengu wa sasa, uchumi wa kidijitali hauna mipaka, vivyo hivyo kwa habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari havina mipaka kwa hiyo, tunamshkuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan kwa kuamua kuunda Wizara hii na kuifanya nchi yetu kuwa moja ya nchi ambazo zina Wizara mahususi katika sekta hizi.”Amesema Yonazi

Kwa upande wake muwakilishi wa TUGHE  Laurencia Masigo amesisitiza umuhimu wa  mafunzo kwa  wafanyakazi ili kuendana na  mabadiliko ya kiteknolojia.

“TUGHE inaipongeza Wizara kwa kupata hati safi kwa mwaka huu, tunawapongeza kwa sababu huo ni mchakato mrefu kuanzia kuweka mikakati na kuifuatilia, kupata fedha na kusimamia kazi mpaka kuja kukaguliwa na Wakaguzi na kupata hati safi, hili ni jambo la kujivunia,''

 

“TUGHE inaomba Watumishi waendelee kupatiwa mafunzo ya muda mfupi na mrefu ili kuweza kuendana na hali halisi ya mabadiliko ya kidijitali”amesema  Masigo..

 

Mwisho.

 

Comments

Dodoma News
Mwanza City, Mwanza, Tanzania
Dennis G. Harrison, mmiliki mwenza wa Mtandao wa Dodoma News Blog, alizaliwa mkoani Morogoro zaidi ya miaka 40 iliyopita. Dennis ana Taaluma ya Uandishi wa Habari (Proffessional Journalism) kutoka Chuo Kikuu cha Mtakatifu Augustine (SAUT). Mwaka 2009 alimaliza Shahada ya Uzamili katika Mawasiliano ya Umma, ikijikita katika Menejimenti ya Uhusiano kwa Umma na Matangazo katika chuo cha SAUT. Mwaka 2002, Dennis aliajiriwa katika Shirika la Posta Tanzania, Ofisi kuu ya Mwanza. Mwaka 2009 aliajiriwa katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Iringa kwa nafasi ya Afisa Habari. Akiwa katika ofisi hiyo alifanya kazi kwa juhudu na maarifa na kufanikiwa kuchaguliwa na wafanyakazi wote kuwa mfanya kazi bora. Kufuatia juhudi na utendaji kazi wake, alipanda hadi nafasi ya Afisa Habari Mwandamizi.