Na. Mwandishi Wetu,
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Hemed
Suleiman Abdulla amesema utekelezaji wa miradi upande wa Zanzibar ni matunda ya
ushirikiano wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (SMT) na Serikali ya
Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ).
![]() |
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Hemed Suleiman Abdulla |
Amesema hayo wakati wa hafla ya utiaji saini wa makabidhiano ya eneo la
mradi kwa ufukwe wa Sipwese, Pemba kwa Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa
Zanzibar iliyofanyika katika ukumbi wa Baraza la Wawakilishi ambapo mradi huo
utatekelezwa na Kampuni ya Dezo Civil Contractors Co. Limited.
Mhe. Hemed alisema kuwa SMZ inafarijika kuona mradi huo unaanza
kutekelezwa kwa vitendo na kwamba utaleta manufaa makubwa kwa wananchi
watakaonufaika na mradi huo.
Pia alitoa pongezi na shukrani kwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango pamoja na Ofisi yake kwa kutoa
ushirikiano mkubwa kwa SMZ.
Amesema Ofisi ya Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
imeonesha dhamira yake ya kusaidia kumaliza tatizo la Mazingira.
Awali Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano) Bw. Abdallah
Hassan Mitawi ambaye alimwakilisha Katibu Mkuu Bi. Mary Maganga, alisema
chimbuko la ujenzi wa eneo hilo ni kupitia ziara ya aliyekuwa Waziri wa Nchi
Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Mussa Azzan Zungu
aliyoifanya mwaka 2019 ambapo aliahidi kusimamia ujenzi wa eneo hilo.
Amesema tathmini katika ufukwe wa Sipwese ilionesha kuwa maji ya bahari
yameingia katika maeneo ya kilimo cha mpunga na wananchi wa Shehia ya Mkungu, Kijiji
cha Sipwese eneo la kwa Mgogo.
Mitawi alisema kujaa kwa maji haya pia yamesababisha kukatika kwa
mawasiliano kutoka upande wa pili takribani kilometa 3.360 ambako ndiko
wananchi wanafuata huduma za jamii kama vile shule hali inayosababisha watoto wa
shule kuvuka maji shingoni kuweza kuifikia shule.
“Mmomonyoko wa fukwe zilizo katika Bahari ya Hindi kwa upande wa
Tanzania Bara na Tanzania Visiwani umeendelea kuwa ni changamoto katika maeneo
mengi ya fukwe na umeanza kuleta athari katika baadhi ya maeneo kwa kusababisha
uharibifu wa miundombinu iliyopo kama vile barabara, majengo, makazi ya watu na
madaraja.
“Hali hii imesababisha Serikali kutumia fedha nyingi katika kukarabati
miundombinu iliyoharibiwa, Fedha ambayo ingeweza kupelekwa katika maeneo
mengine muhimu kwa ajili ya maendeleo ya kiuchumi na kijami,” alisema Mitawi.
Kwa upande wake Katibu Mkuu Afisi ya Makamu wa Pili wa Rais Bw. Thabit
Idarous Faina alisema ujenzi wa eneo hilo utasaidia changamoto inayowakabili
wananchi wa eneo la Sipwese ikiwemo kuvuka kutoka sehemu moja kwenda sehemu
nyengine, maji ya chumvi kuingia katika eneo la kilimo pamoja na kupungua kwa
eneo la makazi ya wananchi.
nimefanya
editing kidogoMakamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Hemed Suleiman Abdulla
amesema utekelezaji wa miradi upande wa Zanzibar ni matunda ya ushirikiano wa
Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (SMT) na Serikali ya Mapinduzi ya
Zanzibar (SMZ).
Amesema hayo wakati wa hafla ya utiaji saini wa makabidhiano ya eneo la
mradi kwa ufukwe wa Sipwese, Pemba kwa Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa
Zanzibar iliyofanyika katika ukumbi wa Baraza la Wawakilishi ambapo mradi huo
utatekelezwa na Kampuni ya Dezo Civil Contractors Co. Limited.
Mhe. Hemed alisema kuwa SMZ inafarijika kuona mradi huo unaanza
kutekelezwa kwa vitendo na kwamba utaleta manufaa makubwa kwa wananchi
watakaonufaika na mradi huo.
Pia alitoa pongezi na shukrani kwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango pamoja na Ofisi yake kwa kutoa
ushirikiano mkubwa kwa SMZ.
Amesema Ofisi ya Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
imeonesha dhamira yake ya kusaidia kumaliza tatizo la Mazingira.
Awali Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano) Bw. Abdallah
Hassan Mitawi ambaye alimwakilisha Katibu Mkuu Bi. Mary Maganga, alisema
chimbuko la ujenzi wa eneo hilo ni kupitia ziara ya aliyekuwa Waziri wa Nchi
Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Mussa Azzan Zungu
aliyoifanya mwaka 2019 ambapo aliahidi kusimamia ujenzi wa eneo hilo.
Amesema tathmini katika ufukwe wa Sipwese ilionesha kuwa maji ya bahari
yameingia katika maeneo ya kilimo cha mpunga na wananchi wa Shehia ya Mkungu,
Kijiji cha Sipwese eneo la kwa Mgogo.
Mitawi alisema kujaa kwa maji haya pia yamesababisha kukatika kwa
mawasiliano kutoka upande wa pili takribani kilometa 3.360 ambako ndiko
wananchi wanafuata huduma za jamii kama vile shule hali inayosababisha watoto
wa shule kuvuka maji shingoni kuweza kuifikia shule.
“Mmomonyoko wa fukwe zilizo katika Bahari ya Hindi kwa upande wa
Tanzania Bara na Tanzania Visiwani umeendelea kuwa ni changamoto katika maeneo
mengi ya fukwe na umeanza kuleta athari katika baadhi ya maeneo kwa kusababisha
uharibifu wa miundombinu iliyopo kama vile barabara, majengo, makazi ya watu na
madaraja.
“Hali hii imesababisha Serikali kutumia fedha nyingi katika kukarabati
miundombinu iliyoharibiwa, Fedha ambayo ingeweza kupelekwa katika maeneo
mengine muhimu kwa ajili ya maendeleo ya kiuchumi na kijami,” alisema Mitawi.
Kwa upande wake Katibu Mkuu Afisi ya Makamu wa Pili wa Rais Bw. Thabit
Idarous Faina alisema ujenzi wa eneo hilo utasaidia changamoto inayowakabili
wananchi wa eneo la Sipwese ikiwemo kuvuka kutoka sehemu moja kwenda sehemu
nyengine, maji ya chumvi kuingia katika eneo la kilimo pamoja na kupungua
kwa eneo la makazi ya wananchi.
Comments
Post a Comment