DODOMA.
Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na
Rushwa (TAKUKURU) mkoa wa Dodoma imesema pamoja na kuhamasisha mapambano dhidi ya vitendo vya rushwa , imepokea malalamiko 133,ambapo taarifa za rushwa
zilikuwa 66 na zisizo za rushwa ni 67.
Taarifa 66 zinazo husu rushwa
zilikuwa za serikali za mitaa 19, elimu 10, polisi 5, mahakama 4, ardhi 4 na sekta
binafsi 4 huku taarifa 11 zikihusu watu binafsi.
Akizungumza na waandishi wa habari
leo mkoani hapa wakati akielezea utekelezaji wa majukumu yao katika robo ya Januari hadi Machi,2022, Mkuu wa Taasisi hiyo Sothenes Kibwengo amesema, taarifa hizo
zinazo husu rushwa zimeshughulikiwa kwa mbinu mbalimbali na kwa mujibu wa sheria
ya kuzuia na kupambana na rushwa.
’’Ambapo uchunguzi wa majalada 16
ulikamilika na mashauri mapya 8 yalifunguliwa na kufanya jumla ya mashauri
yanayoendelea mahakamani 58. Kati ya taarifa 67 zisizohusu rushwa 2
zilihamishiwa idara zingine na wahusika wa taarifa 65 zilizo salia walishauriwa
mahali sahihi pa kuziwasilisha.’’amesema Kibwengo
Pamoja na hayo, Kibwengo amebainisha
kuwa eneo la utoaji huduma linaonekana kulalamikiwa kuwa na viashiria vya
rushwa ,TAKUKURU hufanya uchambuzi wa mfumo ili kubaini iwapo kuna mianya ya
rushwa na kushauri namna ya kuiziba.
‘’Katika eneo hili tumefanya
uchambuzi sita za mifumo katika sekta za mapato,elimu pamoja na ujenzi.Tumebaini
kwamba pamoja na mambo mengine kuna utitiri wa leseni za uchimbaji wa madini
ujenzi .lakini maeneo mengi hakuna inachoendelea na hvyo kuzinyima halmashauri
mapato. Mfano wilayani Mpwapwa kuna leseni za wachimbaji 773 lakini
zinazotumika ni 57 tu.’’ amesema Kibwengo
‘’Pia halmashauri zinapoteza mapato
katika maeneo ambayo uchimbaji unafanyika kiholela na ambayo hayana mashine za
kieletroniki za kukusanya ushuru POS.’’ ameongeza Kibwengo
Akizungumzia kwenye uchambuzi wa
mfumo wa viashiria vya rushwa ya ngono katika sekta ya elimu ngazi ya
halmashauri, amesema imebainika kuwa maeneo hatarishi kwa uwepo wa rusha ya ngono ni
katika upangaji wa vituo vya kazi kwa asilimia 72 na uhamisho ndani ya
halmashauri kwa asilimia 63.
‘’Kwenye uchambuzi wa mfumo wa ujenzi
wa shule shikizi imebainisha kuwa kuna ufahamu ndogo kwa kamati za shule kuhusu
matumizi ya mfumo wa manunuzi ya force account’. Warsha tano za kujadili matokeo
ya uchambuzi wa mifumo kwa kushirikisha wadau zilifanyika katika sekta za elimu
na ujenzi. Ambapo maazimio ya namna ya kuziba mianya ya rushwa yalifikiwa na
muda wa utekelezaji kuwekwa.’’ amesema Kibwengo
‘’Vilevile, taarifa mbili za
utekelezaji wa maazimio yaliyofikiwa siku za nyuma katika sekta za ardhi za
afya zilipokelewa. Tunawakumbusha wote wenye majibu wa kufanyia kazi maazimio
ya kuziba mianya ya rushwa bainishwa kutekeleza wajibu wao kwa wakati.’’ amesema Kibwengo
Mwisho.

Comments
Post a Comment