Na. Kadala Komba Dodoma
Mbunge wa Viti Maalumu Khadija Shaaban Taya maarufu kama
Keisha kwa kushirikiana na Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana, Ajira na Wenye
Ulemavu,
Mbunge wa Viti Maalumu Khadija Shaaban Taya akikabidhi zawadi |
Keisha Akizungumza ngumza hayo alipotembelea shule hiyo na kujioneya mazingira wanayohishi watu wenye ulemavu, Alisema ni furaha kubwa Sana Mimi kuwepo hapa katika kipindi hiki cha mwezi mtukufu wa Ramadhani, kwa kutambua hili tumekuja kuwaona nataka mtambue kuwa Serikali anawakumbuka na kuwathamini tumekuja na hivi vitu hili kuonesha kwamba tupo pamoja.
Pia Keisha Alisema kazi ya mbunge ni kupaza sauti ya Changamoto ambazo
wananchi wanakumbana nazo,Lengo la sisi kuja hapa ni kujua Changamoto
mnazopitia mazingira mnayohishi na hivyo vyote tumekwisha viona tutavifanyia
kazi. Mimi ni kama nyinyi nimesoma Kama nyinyi zingatieni masomo mtafika mbali.
Aidha Keisha alitumia nafasi hiyo kuipongeza Serikali ya hawamu ya sita
chini ya Rais Samia kwa kusikia kilio Cha watu wenye ulemavu wa Ngozi na
kutenga Bajeti ya mafuta ya Ngozi kwa watu wenye Ualbino Alisema ninafuraha
kuona Sasa tumepata mafuta ambayo yatatuweka salama,tumepata mafuta Amini
na kofia pia zinakuja.
Kwa upande wake Prof. Jamal Adam Katundu
Katibu Mkuu Ofisi ya Wziri Mkuu Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu
Ametoa maagizo kwa Mkurugenzi kitengo Cha watu wenye Ulemavu Rasheed
Maftah , kuwapa kipaombele Cha Ajira walimu wanaojitolea katika
shule ya watu wenye ulemavu ya msingi Hombolo Bwawani.
Alisema Chukua idadi ya walimu wanaojitolea kufundisha katika
shule hii wenye sifa, hili wapewe kipaombele kwenye Ajira pindi nafasi za Ajira
zitakapotoka wao wapewe kipaombele .
Pia Katibu Alisema hawa watu wameonesha Moyo wa uzalendo na utayari wa
kufanya kazi tusiwaache tuwape Ajira hili nao waone thamani ya kile
wanachokifanya .
Sambamba na Hilo Mkuu msaidizi wa shule hiyo Bw.Musa Simoni
amemshukuru Mbunge Keisha pamoja na Ofisi ya Waziri Mkuu kwa zawadi ambazo
wametoa kwajili ya watoto wetu wenye ulemavu,sisi Kama Walimu kazi yetu
ni kuhakikisha hivi vitu vinawafikia walengwa, hawahaidi hivi vitu vyote
ambavyo vimeletwa ikiwemo Fedha kutoka kwa Ofisi ya Waziri Mkuu imefika na
itawafikia watoto waliolegwa.
Aidha Bw.Musa Alisema katibu wetu Mkuu ni msikivu tunamwomba asituache
kwani Changamoto ni nyingi katika shule hii, mazingira ya shule sio rafiki kwa
watu wenye mahitaji Muhimu Kama hawa na wewe ni shahidi umejionea Bweni
wanarolala watoto wetu tunaomba mtusaidie.
MWISHO
Comments
Post a Comment