Na. Mwandishi Wetu,
Bodi ya Ushauri ya Wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini TARURA imefanya ukaguzi wa mradi wa ujenzi wa Barabara za Mji wa Serikali Mtumba Jijini Dodoma unaotekelezwa na Mkandarasi China Heinan International Group Co Ltd (CHICO) ambapo kwa awamu ya kwanza mradi huo umekamilika kwa asilimia 100.
Akizungumza katika ukaguzi huo Mwenyekiti wa Bodi ya Ushauri ya TARURA
Mhandisi Florian Kabaka ameeleza kazi ziliyofanyika ni nzuri huku akitoa wito
kwa wananchi kuhakikisha wanalinda miundombinu ya barabara ili iweze kutumika
kama ilivyokusudiwa.
‘‘Tumebaini changamoto baadhi ya watu wasio waaminifu kuiba miundombinu
ya barabara zikiwemo taa, suala hili halipendezi, natoa wito kwa
Menejimenti kuwasiliana na Serikali ya Mkoa, Wilaya pamoja na Kata ili kuweka
mikakati wa kulinda miundombinu hii na kuchukua hatua kali kwa
watakaobainika kuhujumu barabara hizi’’, alisema Mhandisi Kabaka.
Naye Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini TARURA, Mhandisi
Victor H. Seff alisema awamu ya kwanza ya ujenzi wa barabara kwa kiwango cha
lami zenye urefu wa Kilomita 51.2 katika Mji wa Serikali Mtumba tayari
imekamilika na sasa Mkandarasi ameanza awamu ya pili itakayo husisha ujenzi wa
barabara za mlisho zenye urefu wa kilomita 7.91.
‘‘Awamu hii ya pili ya ujenzi wa Barabara za Mlisho zenye urefu wa
kilomita 7.91 utatumia muda wa miezi 8 hadi kukamilika ambapo hadi sasa tayari
Mkandarasi yupo Site”.
Wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini TARURA unaendelea kutekeleza
miradi mbalimbali nchini ikiwa ni pamoja na kufungua barabara kuwezesha
wananchi kufika kusiko fikika.
MWISHO
Comments
Post a Comment