WAZIRI DKT. NDUMBARO ATETA NA BALOZI WA MAREKANI NCHINI, DKT. DONALD WRIGHT KUHUSU UWEKEZAJI MAHIRI KATIKA MAENEO YA WANYAMAPORI (SWICA)
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Damas Ndumbaro leo amekutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Marekani Nchini, Dkt. Donald Wright kuhusu masuala mbalimbali ya Uwekezaji Mahiri katika Vitalu vya Uwindaji wa Wanyamapori
Katika mazungumzo hayo Waziri, Dkt. Ndumbaro amemueleza Balozi huyo kuwa Tanzania
itaendelea kuweka mazingira rafiki ya Uwekezaji kwa Wawekezaji wa kutoka
Marekani hususani katika sekta ya Uwindaji wa Kitalii kwa kuzingatia
maslahi ya nchi.
"Moja ya shabaha yetu kama Wizara ni kuwavutia
Wawekezaji, tunafanya kila liwezekanalo ili kuhakikisha Wawekezaji wa kutoka
nchi mbalimbali wakiwemo wa Marekani wanawekeza katika uwekezaji huu wa muda
mrefu'' amesisitiza Dkt. Ndumbaro
Wizara ya Maliasili na Utalii inatarajia kukusanya
Sh23 bilioni kwa mwaka kutokana na uwekezaji mahiri unaoendekea kufanywa kwenye
sekta ya utalii nchini
MWISHO
Comments
Post a Comment