Na. Zuena Msuya, DSM
Naibu
Katibu Mkuu Wizara ya Nishati, Kheri Mahimbali amefanya ziara ya kushtukiza ya
kukagua eneo la kupakua Mafuta kutoka kwenye Meli kuingia bandarini katika kina
kirefu cha Bahari eneo la Kigamboni jijini Dar es salaam.
Mahimbali
amefanya ziara hiyo, Machi 29, 2022 kwa lengo la kujionea shughuli
zinavyofanyika katika eneo hilo pamoja na mazingira ya kufanyia kazi.
Akiwa
katika ziara hiyo alikutana na baadhi ya wafanyakazi katika eneo hilo na
kuwaeleza kuwa serikali ya inaendelea kuimarisha na kuboresha sekta ya mafuta
nchini ili iweze kuleta tija zaidi kwa taifa na wananchi wake.
Aidha, aliwasisitiza wafanyakazi hao
kufanya kazi kwa weledi wakizingatia maslahi mapana na nchini yetu.
Picha
mbalimbali zikionyesha ziara ya Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Nishati (mwenye
miwani) katika eneo la upakuaji mafuta katika kinakirefu cha bandari Kigamboni
mkoani Dar es Salaam
MWISHO
Comments
Post a Comment