Na. Rhoda Simba, Dodoma.
WAZIRI wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Hamad Masauni ametoa
miezi sita kwa wamiliki wa maroli na mabasi waliotoa vidhibiti mwendo
kuvirejesha katika magari hayo huku ikitangaza operesheni kali ya usalama
barabarani na hatua kali kwa watakao kaidi.
![]() |
Waziri Hamad Masauni |
Waziri Masauni ametoa agizo hilo jijini
hapa wakati akizungumza na waandishi wa habari ambapo amesema lengo
la agizo hilo ni kudhibiti mfululizo wa matukio ya ajali ambazo zimekuwa
zikitokea.
Amesema kutokana na utafiti uliofanywa na Chuo
Kikuu cha Dar es Salaam(UDSM) kwa miaka kadhaa iliyopita ilionesha kuwa
asilimia 76 ya ajali zote husababishwa na vyanzo vya binadamu ikiwemo uzembe,
jambo jingine ni ubovu wa magari ambapo huchangia kwa asilimia nane huku ubovu
wa miundombinu ukichangia kwa asilimia 16.
"Maelekezo ambayo nitayatoa leo hapa ni kupata
suluhisho la ajali hapa nchi na kwa kuanza nataka mabasi na maroli yawe na
vidhibiti mwendo na ndio sheria inavyotaka lakini tumeshuhudia baadhi ya
wamiliki wa magari wanapoingiza vyombo vyao wamekuwa wakitoa,"amesema
Waziri Masauni amesema dhamira ya wanaotoa vifaa
hivyo ni kutaka kuvunja sheria kwasababu vifaa hivyo vimewekwa kwa lengo la
kudhibiti mwendo ili gari lisitembee kwa mwendo usiozidi kilometa 80 kwa saa.
"Hii ni sheria ambayo ipo na tunataka sasa
hivi sheria hii isimamiwe kwahiyo maelekezo yangu kwa jeshi la polisi ni
kusimamia sheria hii na kwa wamiliki wa magari ambao watakiuka sheria hii hatua
stahiki zichukuliwe dhidi yao na kwa wale ambao wanatarajia kuingiza mabasi yao
au maroli waachane kabisa na na mawazo ya kutoa speed Govornor na kwa wale
waliotoa tunatoa muda wa miezi sita wawe wamerejesha vifaa hivyo,"amesema.
Katika hatua nyingine Waziri masauni alitaja chanzo
cha ajali iliyotolea morogoro na kusababisha vifo vya watu zaidi ya 22 amesema
kama lingekuwa na ubora lisingeweza kusababisha vifo vya watu wengi kama
ilivyotokea.
"Ile gari ilikuwa imefungwa vifaa ambavyo
hutumika kuweka zege katika nyumba hivyo ndio vilikata viungo vya watanzania
wenzetu na hapa natoa maelekezo kufanya uchunguzi ili kubaini kiwanda
kilichotumika kutengeneza gari hiyo na kufanya msako nchi nzima kwa kiwanda
kinachofanya vitu vya ovyo kuwakamata na kuwachukulia hatua,"amesema
Ameongeza kuwa:"Hatuwezi kucheza na maisha ya
watanzania hatuwezi kukubali kupoteza maisha ya watu wengi kwasababu ya malsai
au uzembe wa watu wachache na serikali imeweka fedha nyingi katika mifumo
halafu watu wengine wanachezea hili jambo halikubaliki,"ameongeza
Aidha masauni ameliagiza jeshi la polisi kuanzisha
operesheni maalumu ya usalama barabarani itakayohusisha dolia ili kurudisha
hali ya nidhamu katika barabara .
Amesema kuongeza kasi ya operesheni kutasaudia
kuongeza ufanisi katika kusimamia sheria .
"Umefika wakati kupitia upya mfumo mzima wa
mzima wa utoaji mafunzo na leseni kwa madereva ili jeshi la polisi likague vyuo
vote vinavyotoa leseni za udereva ili kubaini kama vinakidhi mahitaji
tuliyonayo ili madereva wanaomaliza wawewanatambua dhamana ya kazi
yao,"amesema
MWISHO
Comments
Post a Comment