Na Mwandishi wetu, Dodoma.
MKUU wa Mkoa wa Dodoma Anthon Mtaka
ameitaka jamii ifundishe watoto kuhusu suala la kutopokea wala kutoa rushwa
wakiwa wadogo ili wanapokua wajue kuwa kitendo hicho si kizuri kwenye maisha
yao.
![]() |
RC Anthony Mtaka |
Mtaka ameyasema hayo jijini
hapa wakati akifungua mafunzo kwa walimu walezi wa klabu za wapinga
rushwa shuleni yaliyoandaliwa na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na
Rushwa (TAKUKURU) ambapo amesema endapo watoto wakifundishwa kuwa vitendo hivyo
si vizuri wakiwa wadogo watakua katika maadili mema.
“Kuna shule ipo Wilaya ya Kondoa
siku tumefika pale wameanza na salamu rushwa ni aduni wa haki ndipo
wanaendelea na salamu nyingine kwahiyo tujitahidi kuwajengea uelewa ili wajue
wakiwa wadogo na siku zote samaki mkunje angali mdogo” amesema Mtaka.
Amesema kuwa elimu ya kutopokea na
kutotoa rushwa itolewe kama ilivyo elimu ya dini itolewayo na
kwa watoto wakiwa wadogo shuleni.
“Wakati wanafunzi wapo shuleni kuna
umoja wakiwa pale kila mmoja na dini yake wanakaa kusali sasa kwanini kama
ilivyo umoja ule tusiwafundishe watoto kujua kuhusu masuala ya rushwa kuwa ni
adui wa haki”amesema Mtaka
Kwa upande wake Kamanda wa
TAKUKURU Mkoa wa Dodoma Sostenes Kibwengo amesema mafunzo hayo
yameandaliwa kwa walimu walezi wa klabu za wapinga rushwa lengo likiwa ni
kujadili namna gani klabu ziimarike na kuwa mfano mzuri
katika kupambana na rushwa.
“lengo ni kujenga kizazi ambacho
kitakuwa na maadili kizazi cha watu ambao ni wazalendo na wanawajibika na wenye
maadili mazuri kwa kufanya hivyo sisi tutakuwa hatuna kazi ya kupiga makelele
achana na rushwa”amesema Kibwengo
Mwisho
Comments
Post a Comment