EURO MILIONI 171 KUTEKELEZA MRADI WA MAJI SIMIYU

Serikali kwa kushirikiana na Benki ya KfW kwa niaba ya Mfuko wa Mabadiliko ya Tabianchi (Green Climate Fund - GCF) inatekeleza mradi wa kukabiliana na Athari za Mabadiliko ya Tabia nchi katika Wilaya tano (5) za Mkoa wa Simiyu ambazo ni Busega, Bariadi, Itilima, Maswa na Meatu. Katika awamu ya kwanza mradi wa maji utatekelezwa katika Wilaya za Busega, Itilima na Bariadi.

 

Katibu Mkuu Wizara ya Maji Mhandishi Anthony Sanga akizungumza na Kamati ya wataalam kutoka sekta mbalimbali zinazohusika katika utekelezaji wa mradi wa maji Simiyu

Akizungumza na Kamati ya Wataamu wa Sekta mtambuka, jijini Dodoma Machi 29, 2022 Katibu Mkuu Wizara ya Maji Mhandishi Anthony Sanga amesema maandalizi ya kuanza utekelezaji wa mradi zinakwenda vizuri na kwamba wako katika hatua za mwisho za kuanza utekelezaji.

 

Mradi huo unakadiriwa kugharimu jumla ya kiasi cha EURO Milioni 171, ambapo GCF watachangia EURO Milioni 102.7, Benki ya KfW itachangia EURO Milioni 26.1, Serikali ya Tanzania EURO Milioni 40.7 na Wananchi kupitia nguvu zao watachangia EURO Milioni 1.5. Hadi mwezi Februari 2022, awamu ya kwanza ya fidia kiasi cha shilingi 1,519,074,522.16 kimelipwa kwa wananchi wapatao 1,201 kati ya 1,308 walio tathiminiwa. Aidha, taratibu za kuwapata wakandarasi kwa ajili ya ujenzi wa mradi zipo katika hatua za mwisho.

 

 

Wataalam kutoka sekta mbalimbali zinazohusika katika utekelezaji wa mradi wakijadili masuala mbalimbali kuhusiana na utekelezaji wa mradi

Picha ya pamoja na wataalam na wadau wa sekta mbalimbali zinazohusika katika utekelezaji wa mradi

Comments

Dodoma News
Mwanza City, Mwanza, Tanzania
Dennis G. Harrison, mmiliki mwenza wa Mtandao wa Dodoma News Blog, alizaliwa mkoani Morogoro zaidi ya miaka 40 iliyopita. Dennis ana Taaluma ya Uandishi wa Habari (Proffessional Journalism) kutoka Chuo Kikuu cha Mtakatifu Augustine (SAUT). Mwaka 2009 alimaliza Shahada ya Uzamili katika Mawasiliano ya Umma, ikijikita katika Menejimenti ya Uhusiano kwa Umma na Matangazo katika chuo cha SAUT. Mwaka 2002, Dennis aliajiriwa katika Shirika la Posta Tanzania, Ofisi kuu ya Mwanza. Mwaka 2009 aliajiriwa katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Iringa kwa nafasi ya Afisa Habari. Akiwa katika ofisi hiyo alifanya kazi kwa juhudu na maarifa na kufanikiwa kuchaguliwa na wafanyakazi wote kuwa mfanya kazi bora. Kufuatia juhudi na utendaji kazi wake, alipanda hadi nafasi ya Afisa Habari Mwandamizi.