DODOMA.
Halmashauri ya Kuu ya Chama cha
Mapinduzi CCM Taifa imemteua Katibu Mkuu
Mstaafu Abdulrahman Omari Kinana kuwa mgombea nafasi ya Makamu Mwenyekiti wa Chama hicho Tanzanzania
Bara.
Uteuzi huo unatokana na aliyekuwa
Makamu Mwenyekiti wa Chama hicho Mzee Philip Mangula kuandika barua ya kung’atuka
katika nafasi hiyo.
Hayo yamesemwa leo jijini Dodoma na
katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama hicho Shaka Hamdu Shaka, wakati akizungumza
na Waandishi wa Habari mara baada ya kumalizika kwa Vikao vya Halmashauri Kuu
Taifa na Kamati kuu kuelekea kwenye Mkutano Mkuu Maalum wa Chama hicho unao
tarajiwa kufanyika Aprili 1,2022 jijini hapa.
‘’Halmashauri kuu ya CCM Taifa leo tarehe 31 Machi 2022, imepokea
barua ramsi ya kung’atuka kwa Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Tanzania
Bara Mzee Philip Japhet Mangula. Ambayo amemuandikia na Mwenyekiti amewasilisha
mbele ya kikao cha Halmashauri Kuu ya Taifa.’’amesema Shaka
‘’Kwa hiyo Halmashauri Kuu ya Taifa imefanya uteuzi wa ndugu
Abdulrahman Omari Kinana Katibu Mkuu mstaafu wa Chama cha Mapinduzi ateuliwe kuwa
mgombea wa nafasi ya Makamu wa Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi.’’ ameongeza Shaka
Hatahivyo, Halmashauri Kuu ya Chama
hicho pia imemsamehe na kumrudishia uanachama Bernad Membe ambaye amewahi kuwa
Waziri wa Mambo ya Nje na kufukuzwa uanachama februari 2020 kwa makosa ya
kinidhamu.
‘’Lakini yuko ndugu mwingine Abdala
Maulid Diwani yuko kule Zanzibar aliwahi kuwa Mjumbe wa Jimbo la Jang’ombe naye
katika kipindi cha mwaka 2018 aliondolewa uanachama wake . Nina furaha
kuwajulisha umma Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi Taifa leo tarehe 31
Machi 2022 imewasamehe na imewarudishi uanachama wao.’’ amesema Shaka
Mwisho.
Comments
Post a Comment