SERIKALI KUBORESHA USHIRIKIANO WA KIMATAIFA

Na. Rhoda Simba, DODOMA

 

KATIBU Mkuu, Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Dkt. Jimmy Yonazi amesema, Serikali itahakikisha inaboresha ushirikiano na mataifa ya nje katika utendaji kazi kuhusu suala zima la ulinzi na usalama ili kukabiliana na vitendo vya uhalifu wa kimtandao.

 

Katibu Mkuu, Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Dkt. Jimmy Yonazi

Ameyasema hayo leo Februari Jijini hapa wakati akifunga mafunzo ya siku tano kwa wapelelezi pamoja na maaskari wa chumba cha mashtaka wa Tanzania na Zanzibar lengo likiwa ni kuwajengea uwezo kuhusu masuala ya uhalifu wa Mtandao.

 

Aidha, Dkt. Yonazi amesema kuwa mafunzo hayo ni muhimu kwaajili yakujenga uwezo wa nchi hivyo jukumu lao ni   kuhakikisha wanalinda usalama wa nchi.

 

“Kama Serikali tutaendelea kufanyia kazi ya mashirikiano baina ya nchi yetu na nchi nyingine katika kuhakikisha tunaimarisha masuala ya mawasiliano ya TEAHAMA ili kukabiliana na uhalifu wa kimtandao,” amesema.

 

Pamoja na mambo mengine amesema uhalifu wa kimtandao ni mpana na kila siku teknolojia inakuwa hivyo ni muhimu kuhakikisha kila mara wanajengeana uwezo ili kwenda na ulimwengu wa kidijitali.

 

Amesema Serikali imechukua hatua kwa kutunga Sheria ya makosa ya mtandao ya mwaka 2015 ili kuweza kukabiliana na masuala ya uhalifu wa kimtandao ambao umekuwa ukishika kasi.

 

Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Mashtaka nchini, DCI Camilius Wambura amesema Mafunzo hayo yataleta matokeo chanya kutokana na mbinu walizopata ili kukabiliana na uhalifu wa kimtandao kwani maarifa yatawasaidia katika kubadilishana taarifa.

 

Wambura amewataka wapelelezi hao pamoja na askari kuhakikisha wanafanya kazi kwa uadilifu na nidhamu katika utendaji kazi wao kwani tabia za wachache zimekuwa zikiharibu taswira ya Jeshi jambo ambalo si jema.

 

Mwisho

 

 

Comments

Dodoma News
Mwanza City, Mwanza, Tanzania
Dennis G. Harrison, mmiliki mwenza wa Mtandao wa Dodoma News Blog, alizaliwa mkoani Morogoro zaidi ya miaka 40 iliyopita. Dennis ana Taaluma ya Uandishi wa Habari (Proffessional Journalism) kutoka Chuo Kikuu cha Mtakatifu Augustine (SAUT). Mwaka 2009 alimaliza Shahada ya Uzamili katika Mawasiliano ya Umma, ikijikita katika Menejimenti ya Uhusiano kwa Umma na Matangazo katika chuo cha SAUT. Mwaka 2002, Dennis aliajiriwa katika Shirika la Posta Tanzania, Ofisi kuu ya Mwanza. Mwaka 2009 aliajiriwa katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Iringa kwa nafasi ya Afisa Habari. Akiwa katika ofisi hiyo alifanya kazi kwa juhudu na maarifa na kufanikiwa kuchaguliwa na wafanyakazi wote kuwa mfanya kazi bora. Kufuatia juhudi na utendaji kazi wake, alipanda hadi nafasi ya Afisa Habari Mwandamizi.