Na. Dennis Gondwe, DODOMA
Wajumbe wa Jukwaa la uwezeshaji wanawake kiuchumi
katika Halmashauri ya Jiji la Dodoma wametakiwa kuchangua viongozi wenye uwezo
wa kuongoza na kuleta maendeleo tofauti na kuchagua kwa kuangalia sura.
Mkuu wa Idara ya Maendeleo ya Jamii na Vijana, Asha Vuai |
Kauli hiyo ilitolewa na Mkuu wa Idara ya Maendeleo ya Jamii
na Vijana Halmashauri ya Jiji la Dodoma, Asha Vuai alipokuwa akifungua mkutano
wa uchaguzi wa viongozi wa Jukwaa la uwezeshaji wanawake kiuchumi Halmashauri
ya Jiji la Dodoma uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa halmashauri hiyo.
Vuai alisema “niwasihi ndugu zangu tutumie nafasi hii
kuchaguia viongozi watakaotuunganisha kama wanawake kwa kutumia changamoto zetu
ili ziweze kutatuliwa. Pia viongozi hao wawe kichocheo cha kutupatia fursa za
kiuchumi zinazopatikana. Hivyo, tuchague viongozi kwa sifa zao siyo sura zao”
alisema Vuai.
Mkuu huyo wa idara alisema kuwa Jukwaa la uwezeshaji
wanawake kiuchumi linalenga kuondoa matabaka na sheria kandamizi ambazo
zitasaidia kuondoa ubaguzi wa kiuchumi. “Kwa wanawake ni jambo muhimu sana
katika kuleta maendeleo ya usawa na pato la taifa kwa ujumba. Ushiriki wa
wanawake katika shughuli za kiuchumi ni kichocheo kizuri cha maendeleo ya nchi
yetu na jamii kwa ujumla. Kwa sabau ushiriki wa wanawake katika uchumi unaleta
mabadiliko makubwa sana katika familia na jamii kwa ujumla” alisema Vuai.
Katika uchaguzi huo nafasi zilizowaniwa ni mwenyekiti,
makamu mwenyekiti, katibu, katibu msaidizi na mweka hazina iliwa ni maandalizi
ya kuelekea maadhimisho ya siku ya wanawake Duniani.
=30=
Comments
Post a Comment