Na Mwandishi Wetu, Dodoma.
Imeelezwa kuwa matumizi yasiyo sahihi ya TEHAMA kwa watoto na
vijana balehe huweza kupelekea ulaghai wa kingono mtandaoni.
Hayo yamesemwa na Mkurugenzi Idara ya Maendeleo ya Watoto kutoka Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalumu Sebastian
Kitiku wakati akizungumza na Cfm.
“wakijiingiza kwenye matumizi yasiyosahihi watarajie yafuatayo,
kwanza wanaweza wakajikuta wanatumiwa jumbe zenye maudhui ya kingono. Sasa
madhara yake ni nini, kwa umri wao wakitumiwa jumbe hizo watakutana na maudhui
ya kingono ambayo yanaweza ya kawaathiri kisaikojia'' amesema Kitiku
Aidha amesema eneo lingine ambalo watoto wanaweza kukumbana
nalo wakitumia mitandao isivyo, ni ulaghai wa kingono mtandaoni ambapo amesema
hao watu ambao ni wahalifu mara nyingine wanatumia vitisho.
“Sasa ulaghai unakujaje, mtoto anaingia kwenye mtandao anakutana
na mtu ambaye hata hamfahamu anamlaghai. Mara nyingine wanaweza wakafanya ngono
kwa njia ya mtandao, lakini vilevile wanaweza wakawasiliana mpaka wakakutana
kwa njia tofauti tofauti'' ameongeza Kitiku
Hata hivyo imeikumbusha jamii kuwa sheria zilizopo zinazuia matumizi ya simu yasiyo sahihi ikiwemo sheria ya mtoto namba 21 ya mwaka 2009 na sheria ya makosa ya mtandao ya mwaka 2015.
Mwisho.
Comments
Post a Comment