Na. OMM Rukwa.
Zaidi
ya shilingi Bilioni 27.5 zimetolewa kwa ajili ya ujenzi na ukarabati wa barabara
zilizo chini ya Wakala za TANROADS na TARURA katika mwaka wa fedha 2021/2022
ikiwa ni ongezeko la kibajeti mara mbili zaidi ya lile la awali kwa mwaka fedha
uliopita.
Kutolewa
kwa fedha hizo kunatajwa kuwa ni moja ya mafanikio makubwa ya serikali ya awamu
ya Sita inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan tangia aingie madaraka takribani
mwaka mmoja hadi sasa.
Akizungumza
katika ufunguzi wa kikao cha 40 Bodi ya Barabara mkoa hii leo (28.02.2022)
mjini Sumbawanga, Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Joseph Mkirikiti amesema fedha hizo
tayari zinaendelea kutekeleza miradi ya barabara kwenye maeneo mbalimbali
mkoani humo.
“Nichukue
fursa hii kuipongeza serikali yetu inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan kwa
kuendelea kutupatia fedha kwa ajili ya kuboresha miundombinu ya barabara zetu
ambapo maendeleo makubwa yanaonekana kote “alisema Mkirikiti.
Mkuu
huo wa Mkoa aliongeza kusema kqti ya fedha hizo shilingi Bilioni 15.2 ni kwa
ajili ya barabara za Tanroads na Bilioni 12.3 ni kwa ajili ya barabara za
Tarura.
Mkirikiti
aliwataka wajumbe wa kikao hicho kufanya tathmini ya kina juu ya matumizi ya
fedha hizo za barabara kwa kuwa zimetolewa na serikali kwa lengo la kuboresha
barabara hususan za vijijini ili zichochee ukuaji wa uchumi .
“Fedha
hizi ni zaidi ya mara tatu ya makusanyo ya halmashauri zetu zote nne. Makusanyo
ya ndani ya halmashauri zetu ni Bilioni takribani 9 katika mwaka 2021/22”
alisema Mkirikiti.
Aidha,
Mbunge wa Kalambo Josephat Kandege aliomba serikali kufanya udhibiti na kulinda
eneo lililotengwa kwa ajili ya ujenzi wa uwanja mpya wa ndege Kisumba ili
wananchi wasilivamie na kwa kilimo na makazi.
Akiwasilisha taarifa ya utekelezaji kazi za barabara kuu za mkoa kwa mwaka 2021/22 na mpango na bajeti kwa mwaka 2022/2023 Meneja wa Tanroad Mkoa wa Rukwa, Mhandisi Mgeni Mwanga alisema asilimia kubwa barabara za mkoa za lami na changarawe zote zilikuwa na hali nzuri.
Mhandisi Mwanga alisema Tanroad inasimamia mtandao wa barabara zenye urefu wa kilometa 1,250.2 ambapo barabara kuu zina urefu wa kilometa 415 kati ya hizo za lami ni (298.35 km) na changarawe (117.51 km) na barabara za mkoa zina jumla ya kilometa 834.98 kati hizo za lami ni (76.8 km) na za changarawe ni (758.1 km).
Mhandisi
Mwanga alisema katika mwaka 2022/2023 bajeti ya matengenezo kupitia Mfuko wa
Barabara inayotarajia kupitishwa na Bunge ni shilingi Bilioni 13.81 ambapo
jumla ya madaraja 32 katika barabara kuu na madaraja 62 katika barabara za mkoa
yatajengwa na kukarabatiwa.
“Barabara
nyingi zaidi zitajengwa na kufanyiwa matengenezo katika mwaka 2022/23 kuliko
miaka iliyopitya na kuisaidia kuinua uchumi wa mkoa” alisisitiza Mhandisi
Mwanga.
Naye
Meneja wa TARURA Mkoa wa Rukwa, Mhandisi Seth Mwakyembe alisema wakala huo
unahudumia mtandao wa barabara wenye urefu wa kilometa 2,304.6 kwenye
halmashauri zote za Manispaa Sumbawanga (476.34 km), Sumbawanga DC (591.39 km),
Nkasi DC (675.25 km) na Kalambo DC (561.28 km).
“Tunapenda
kuishukuru serikali kwa kuendelea kubuni vyanzo vipya vya mapato
vinavyoiwezesha Tarura kutekeleza majukumu yao vema ambapo tayari serikali
imetoa Bilioni 12 zinaendelea kutumika katika mwaka 2021/2022” alisema Mhandisi
Mwakyembe.
Akichangi
katika kikao hicho Mkuu wa TAKUKURU Mkoa wa Rukwa Daniel Ntera alitoa ushauri
kwa TARURA na TANROAD kuacha kutoa kazi kwa wakandarasi wasio na uwezo li kazi
za ujenzi barabara uende kwa kasi na ubora.
Ntera
aliongeza kusema changamoto nyingine iliyopo mkoa wa Rukwa ni kwa wahandisi wa
TARURA wa wilaya za Nkasi na Kalambo kutofuatiliana na kusimamia kikamilifu
miradi ya barabara.
“Mkandarasi
mmoja kupewa kazi nyingi kwa wakati mmoja wakati uwezo wake ni mdogo hakipaswi
kiendelee kwani kinachelewesha utekelezaji wa miradi hivyo ni vema kazi
zitolewe kwa wenye uwezo” alisema Ntera.
Mbunge
wa Sumbawanga Mjini Aishi Hilaly alitoa ushauri kwa viongozi wenzake kuacha
kuomba kazi za ujenzi wa barabara ndani ya mkoa wa Rukwa ili kuwezesha
watendaji kuwa na usimamizi mzuri.
“Tuna
viongozi wanaomba kazi ndani ya Rukwa hatua inayokwamisha watendaji kufanya
usimamizi wa barabara.Nashauri sisi tukaombe nje ya Rukwa” alisema Aeshi.
Mkuu wa Wilaya ya Nkasi, Peter Lijuakali akifuatlia majadiliano leo kwenye kikao cha Bodi ya Barabara mkoa wa Rukwa kinachofanyika mjini Sumbawanga Kaimu Katibu Tawala Mkoa wa Rukwa Dkt. Boniface Kasululu akizungumza leo kwenye kikao cha Bodi ya Barabara cha Mkoa wa Rukwa kilichofanyika leo mjini Sumbawanga
Mwisho
Comments
Post a Comment