Mtaka:Siwezi kujenga madarasa ,tulete madawati ushindwe kuleta mtoto shule

 





Na Mwandishi Wetu, Dodoma.

Mkuu wa mkoa wa Dodoma Antony Mtaka, ameagiza kukamatwa kwa wazazi na walezi 88 wa watoto ambao hawajiripoti  kuanza na masomo ya kidato cha kwanza katika shule ya sekondari iliyopo mkoani hapa.

Tangu kufunguliwa kwa shule januari 17,2022 shule hiyo imepokea wanafunzi 67 pekee licha ya wanafunzi 165 kufaulu kujiunga na shule hiyo.

Mkuu huyo wa mkoa ametoa maagizo hayo leo wakati akizungumza na wazazi,walimu na wanafunzi wa shule ya hiyo.



''Siwezi kujenga madarasa ,tulete madawati ushindwe kuleta mtoto. Haiwezekani, haiwezekani.  Nitafanya msako ile saa tisa  usiku nyumba kwa nyumba .Tumesema leta mtoto hata kama hana sare za shule. Unambeba mtoto unampeleka kwenda  kibarua mjini'' amesema Mtaka

Hatahivyo, mwaka jana shule hiyo katika matokeo ya kidato cha nne ilishika nafasi ya 51 kati ya shule 52.

Mwisho.


Comments

Dodoma News
Mwanza City, Mwanza, Tanzania
Dennis G. Harrison, mmiliki mwenza wa Mtandao wa Dodoma News Blog, alizaliwa mkoani Morogoro zaidi ya miaka 40 iliyopita. Dennis ana Taaluma ya Uandishi wa Habari (Proffessional Journalism) kutoka Chuo Kikuu cha Mtakatifu Augustine (SAUT). Mwaka 2009 alimaliza Shahada ya Uzamili katika Mawasiliano ya Umma, ikijikita katika Menejimenti ya Uhusiano kwa Umma na Matangazo katika chuo cha SAUT. Mwaka 2002, Dennis aliajiriwa katika Shirika la Posta Tanzania, Ofisi kuu ya Mwanza. Mwaka 2009 aliajiriwa katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Iringa kwa nafasi ya Afisa Habari. Akiwa katika ofisi hiyo alifanya kazi kwa juhudu na maarifa na kufanikiwa kuchaguliwa na wafanyakazi wote kuwa mfanya kazi bora. Kufuatia juhudi na utendaji kazi wake, alipanda hadi nafasi ya Afisa Habari Mwandamizi.