Waziri wa Mambo ya ndani ya nchi,
Mhandisi Hamad Masauni ameunda kamati itakayo toa ushauri kwa serikali kuwa nini
kifanyike ili kupata suluhisho la kudumu la matatizo ya matukio ya mauji yanayo
tokea hapa nchini.
Aidha, ameipa kamati hiyo siku 21, kuweza
kuishauri serikali kuja na mkakati wa kitaifa wa kuhakikisha kwamba changamoto
hiyo inadhibitiwa.
Masauni ameyasema hayo leo jijini
Dodoma ,wakati akizungumza na waandishi wa habari, ambapo amesema katika kipindi
cha mwezi mmoja matukio 179 ya mauaji yametokea huku walio jihusisha na matukio
hayo wakiwa ni zaidi ya 150.
‘’Ni lazima kila ambaye ameshiriki
kwenye mauaji ya mtu yeyote katika nchi hii lazima akamatwe’’ amesema Masauni
Akitaja vyanzo vya mauji mauaji hayo
kuwa ni kugombania mali, wivu wa mapenzi,visasi,ushirikina,migorogoro ya ardhi,
ulevi na kujichukulia sheria mkononi huku akibainisha mikoa vinara ambayo
inaongoza kutekeleza matukio ya mauaji hayo.
‘’ ’Kwa mujibu wa utafiti wetu wa
haraka haraka tumeona kuna mikoa ambayo ndiyo vinara Kagera, Dodoma, Tabora, kigoma
na Songwe’’ ameongeza Masauni
Mwisho.
Comments
Post a Comment