MASAUNI AITAKA UNHCR KUFUATA SHERIA, MWAKILISHI MKAZI MPYA AJITAMBULISHA KWA WAZIRI, AIPONGEZA SERIKALI KWA KUPOKEA, KUHIFADHI WAKIMBIZI NCHINI

 Na WMNN, Dar es Salaam.

WAZIRI wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, amelitaka Shirikika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi (UNHCR) nchini kufanya kazi kwa kuzingatia sera, sheria na vipaumbele vya Serikali katika utendaji wake.

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (kushoto), akizungumza na Mwakilishi Mkazi wa Shirikika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi (UNHCR) Nchini, Mahoua Bamba Parums, kuhusu masuala mbalimbali ya wakimbizi, katika Kikao kilichofanyika Ofisi ndogo ya Wizara, jijini Dar es Salaam


Masauni amezungumza hayo jijini Dar es Salaam, leo, katika Kikao na Mwakilishi Mkazi mpya wa Shirikika hilo Nchini, Mahoua Bamba Parums, ambaye alifika ofisini kwa Waziri huyo kwa lengo la kujitambulisha baada ya kuwasili nchini mwishoni mwa mwaka jana.

“Karibu sana Tanzania na pia nakupongeza sana kwa kuteuliwa katika nafasi hii, natumai kupitia Shirika lako hapa nchini tutafanya kazi vizuri kwa kuzingatia sera, sheria na vipaumbele vya serikali katika utendaji wako,” alisema Masauni.

Kwa upande wake Mwakilishi Mkazi huyo, Mahoua, pia alimpongeza Waziri huyo kwa kuteuliwa kwenye nafasi hiyo kuiongoza  Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (kushoto), akimsindikiza Mwakilishi Mkazi wa Shirikika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi (UNHCR) Nchini, Mahoua Bamba Parums, baada ya kumaliza mazungumzo yao kuhusu masuala mbalimbali ya wakimbizi, katika Kikao kilichofanyika ofisi ndogo ya Wizara, jijini Dar es Salaam


“Nakupongeza Mheshimiwa Waziri kwa kuteuliwa kwa kuteuliwa kuwa Waziri na pia naipongeza Tanzania kwa ukarimu wake wa kuendelea kupokea na kuhifadhi wakimbizi kwa miaka mingi sasa na naomba muendelee kufanya hivyo,” alisema Mahoua.

Pia Mwakilishi Mkazi huyo alimuhakikishia Waziri kuendeleza ushirikiano katika shughuli za hifadhi ya wakimbizi na UNHCR itaendelea kushirikiana na Serikali ya Tanzania katika kuwahudumia Wakimbizi.

Mwisho

Comments

Dodoma News
Mwanza City, Mwanza, Tanzania
Dennis G. Harrison, mmiliki mwenza wa Mtandao wa Dodoma News Blog, alizaliwa mkoani Morogoro zaidi ya miaka 40 iliyopita. Dennis ana Taaluma ya Uandishi wa Habari (Proffessional Journalism) kutoka Chuo Kikuu cha Mtakatifu Augustine (SAUT). Mwaka 2009 alimaliza Shahada ya Uzamili katika Mawasiliano ya Umma, ikijikita katika Menejimenti ya Uhusiano kwa Umma na Matangazo katika chuo cha SAUT. Mwaka 2002, Dennis aliajiriwa katika Shirika la Posta Tanzania, Ofisi kuu ya Mwanza. Mwaka 2009 aliajiriwa katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Iringa kwa nafasi ya Afisa Habari. Akiwa katika ofisi hiyo alifanya kazi kwa juhudu na maarifa na kufanikiwa kuchaguliwa na wafanyakazi wote kuwa mfanya kazi bora. Kufuatia juhudi na utendaji kazi wake, alipanda hadi nafasi ya Afisa Habari Mwandamizi.