Dk. Jafo: Pandeni mikoko kwa wingi


Na. Mwandishi Wetu,

Wakazi wa Kijiji cha Mbuchi, Tarafa ya Mbwela, Wilaya ya Kibiti wametakiwa kupanda miti aina ya mikoko katika Delta ya Mto Rufiji ili kulinda miundombinu inayojengwa na Serikali kwa gharama kubwa ikiwa ni pamoja na ujenzi wa daraja unaoendelea katika Kijiji cha Mbuchi.

 


Wito huu umetolewa mwishoni mwa wiki na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Dkt. Selemani Jafo baada ya kuzindua kampeni ya upandaji miti aina ya mikoko katika kijiji cha Mbuchi.

Dkt. Jafo amewata wakazi wa Mbuchi kuongeza kasi ya upandaji miti aina ya mikoko kwa lengo la kupunguza kasi ya maji na mmomonyoko wa ardhi pembezoni mwa daraja linalojengwa katika Kijiji cha Mbuchi sambamba na kuhifadhi mazingira

Amesema Serikali inatenga fedha nyingi kwa ajili ya kuboresha miundombinu na kutolea mfano wa barabara na madaraja, hivyo wananchi wana wajibu wa kuhakikisha wanakuwa walinzi namba moja wa rasilimali hizo na kuwabaini wahujumu ili waweze kuchukuliwa hatua kwa mujibu wa Sheria.

"Uimara wa daraja hili linalojengwa hapa Mbuchi utategemea sana uhifadhi wa mazingira yetu, tupande mikoko kwa wingi" Alisisitiza Dkt. Jafo.



Pia amesema Serikali imezindua kampeni ya upandaji miti katika ngazi ya kaya na wanafunzi mashuleni. "Tumezindua kampeni ya upandaji miti ambapo kila kaya inatakiwa kupanda na kutunza miti walau mitatu (3) na mti mmoja (1) kwa kila mwanafunzi" Alifafanua Dkt. Jafo.

Nae Mkuu wa Wilaya ya Kibiti, Kanali Ahmed Abbas Ahmed amesema kuwa zaidi ya nusu ya mikoko yote inayopatikana Tanzania iko katila Delta ya Rufiji hivyo kupitia kamati za ulinzi katika ngazi zote watahahikisha kasi ya upandaji wa mikoko na ulinzi unaimarika.




 

Comments

Dodoma News
Mwanza City, Mwanza, Tanzania
Dennis G. Harrison, mmiliki mwenza wa Mtandao wa Dodoma News Blog, alizaliwa mkoani Morogoro zaidi ya miaka 40 iliyopita. Dennis ana Taaluma ya Uandishi wa Habari (Proffessional Journalism) kutoka Chuo Kikuu cha Mtakatifu Augustine (SAUT). Mwaka 2009 alimaliza Shahada ya Uzamili katika Mawasiliano ya Umma, ikijikita katika Menejimenti ya Uhusiano kwa Umma na Matangazo katika chuo cha SAUT. Mwaka 2002, Dennis aliajiriwa katika Shirika la Posta Tanzania, Ofisi kuu ya Mwanza. Mwaka 2009 aliajiriwa katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Iringa kwa nafasi ya Afisa Habari. Akiwa katika ofisi hiyo alifanya kazi kwa juhudu na maarifa na kufanikiwa kuchaguliwa na wafanyakazi wote kuwa mfanya kazi bora. Kufuatia juhudi na utendaji kazi wake, alipanda hadi nafasi ya Afisa Habari Mwandamizi.