WIZARA YA ARDHI YAKUSANYA ZAIDI YA BILIONI 60 YA KODI YA PANGO LA ARDHI

 


Na Mwandishi Wetu, Dodoma.

Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi imesema kuwa kwa mwaka  huu imeweza  kukusanya zaidi ya bilioni 60 ya kodi ya pango la ardhi.

Hayo yamesemwa leo jijini Dodoma na Mkuu wa kitendo cha kodi katika wizara hiyo Bwana Denis Masami ,wakati wakitoa taarifa kwa vyombo vya habari kuhusu wajibu wa ulipaji kodi kwa mujibu wa sheria zilizopo’’ Hadi sasa tumekusanya zaidi ya bilioni 60, kipindi hiki ndio msimu wetu wa ukusanyaji’’

Kwa upande wa Kamshina wa Ardhi  Nathaniel Mathew Nhonge amesema kila mwaka  mwananchi anawajibu wa kulipia pango la ardhi na kusisitiza kuwa, muda wa kulipia kodi hiyo bado upo na kwa atakaye chelewa kulipia kwa wakati atatozwa riba.



‘’Kwahiyo tumeamua kuwaambia wananchi muda wa kulipa kodi bila riba bado upo leo ni tarehe 30, tarehe 31 ambacho ni kipindi kizuri cha kulipa bila riba’’

Wakati huo huo ,amesema kulipa kodi ni wajibu wa kila  mtanzania kwa mujibu wa sheria maadam amemilikishwa hati ya kumilikishwa ardhi.

Sheria Na.4 ya mwaka 1999 sehemu ya 33 aya ya 11 imetoa mwanya kwa walipa kodi kuendelea kulipa bila adhabu hadi tarehe 31 Desemba ya mwaka unaohusika. Baada ya hapo adhabu inatozwa.

Comments

Dodoma News
Mwanza City, Mwanza, Tanzania
Dennis G. Harrison, mmiliki mwenza wa Mtandao wa Dodoma News Blog, alizaliwa mkoani Morogoro zaidi ya miaka 40 iliyopita. Dennis ana Taaluma ya Uandishi wa Habari (Proffessional Journalism) kutoka Chuo Kikuu cha Mtakatifu Augustine (SAUT). Mwaka 2009 alimaliza Shahada ya Uzamili katika Mawasiliano ya Umma, ikijikita katika Menejimenti ya Uhusiano kwa Umma na Matangazo katika chuo cha SAUT. Mwaka 2002, Dennis aliajiriwa katika Shirika la Posta Tanzania, Ofisi kuu ya Mwanza. Mwaka 2009 aliajiriwa katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Iringa kwa nafasi ya Afisa Habari. Akiwa katika ofisi hiyo alifanya kazi kwa juhudu na maarifa na kufanikiwa kuchaguliwa na wafanyakazi wote kuwa mfanya kazi bora. Kufuatia juhudi na utendaji kazi wake, alipanda hadi nafasi ya Afisa Habari Mwandamizi.