WANANCHI JIJI LA DODOMA WANATARAJIA HUDUMA BORA

Na. Dennis Gondwe, DODOMA

WANANCHI wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma wanatarajia huduma bora kutoka kwa taasisi mbalimbali ikiwa ni utekelezaji wa dhana ya uwajibikaji katika utoaji wa huduma bora.

Meya wa Jiji la Dodoma, Prof. Davis Mwamfupe (kulia) akipokea zawadi kutoka kwa Meneja wa Tawi la NMB Dodoma, Amos Mubusi


Kauli hiyo ilitolewa na Mstahiki Meya wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma, Prof. Davis Mwamfupe baada ya kupokea zawaidi ya mwaka mpya kutoka benki ya NMB ofisini kwake.

Prof Mwamfupe alisema “Halmashauri ya Jiji la Dodoma na benki ya NMB zinategemeana katika maeneo mbalimbali. Wananchi wanategemea huduma bora kutoka kwetu, hivyo, tunawajibu wa kuendelea kutoa huduma bora kwa wananchi wetu”.

 

MWISHO

Comments

Dodoma News
Mwanza City, Mwanza, Tanzania
Dennis G. Harrison, mmiliki mwenza wa Mtandao wa Dodoma News Blog, alizaliwa mkoani Morogoro zaidi ya miaka 40 iliyopita. Dennis ana Taaluma ya Uandishi wa Habari (Proffessional Journalism) kutoka Chuo Kikuu cha Mtakatifu Augustine (SAUT). Mwaka 2009 alimaliza Shahada ya Uzamili katika Mawasiliano ya Umma, ikijikita katika Menejimenti ya Uhusiano kwa Umma na Matangazo katika chuo cha SAUT. Mwaka 2002, Dennis aliajiriwa katika Shirika la Posta Tanzania, Ofisi kuu ya Mwanza. Mwaka 2009 aliajiriwa katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Iringa kwa nafasi ya Afisa Habari. Akiwa katika ofisi hiyo alifanya kazi kwa juhudu na maarifa na kufanikiwa kuchaguliwa na wafanyakazi wote kuwa mfanya kazi bora. Kufuatia juhudi na utendaji kazi wake, alipanda hadi nafasi ya Afisa Habari Mwandamizi.