Na Mwandishi Wetu, Dodoma.
Tume ya Utumishi wa Walimu TSC imesema kuwa pamoja na
changamoto za walimu bado viwango vya ufaulu katika shule za msingi na
sekondari vimeongeka kutokana na walimu kufanya kazi kwa moyo wa kujitolea.
Kauli hiyo imetolewa leo jijini Dodoma na Mwenyekiti wa Tume
hiyo Profesa Willy Komba ,wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu
masuala ya maadili kwa walimu.
‘’Kama Tume tunaridhishwa na kazi wanayoifanya walimu nchini
kote, pamoja na changaoto za walimu bado viwango vya ufaulu katika shule za
msingi na sekondari zimekukwa zikiongezeka kutokana na walimu kufanya kazi kubwa
kwa moyo’’ amesema
Wakati huo huo, Profesa Wiily amempongeza Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Samia Hassan kwa kuendelea kuunga mkono sekta ya elimu na tangu aingie
madarakani walimu wamepanda madaraja.
‘’Walimu laki moja ishirini na sita elfu na mia tatu arobaini
na sita waliokuwa na sifa za kupanda
madaraja walipanda madaraja. Hakuna
aliyeachwa. Walimu waliopandishwa walirekebishiwa mishahara yao kwa wakati’’
amesema
Profesa Willy amesema, pamoja na kazi nzuri zilizofanywa na walimu
zipo kasoro ambazo zilijitokeza ikiwemo baadhi ya walimu kukiuka maadili ya
utumishi wa walimu.
‘’Kazi ya ualimu ikiacha maadili pembeni haijakamilika,
mwalimu lazima awe muadilifu ,tunapozungumzia kazi yake kuna maadili mahususi
yanayolenga mwalimu, wajibu wa mwalimu ,namna gani mwalimu anapaswa kufanya’’
amesema
Ameongeza kuwa ‘’ Ni haki ya mtoto kulelewa, ni wajibu wa mwalimu
kumlea kimwili, kuhakikisha kwamba anakauwa salama, atamkinga na madhila ya
kimazingira, kama ubakaji, ulawiti, madawa ya kulevya. kwahiyo tunaposikia
amejishusiha kimapenzi na mwanafunzi hajatimiza wajibu wake, kwahiyo anapaswa
kumlea kimwili na kumuepusha na madhara hayo ili kumuepusha’’ amesema
Akizungumza vitendo vya ukiukwaji wa maadili Profesa Willy
amesema katika kipindi cha mwaka 2020/2021 yapo mambo ambayo baadhi ya walimu
waliyafanya ikiwemo utoro, kughushi vyeti, ukaidi, ulevi pamoja na uhusiano wa
kimapenzi.
‘’Utoro kwa walimu unashika nafasi ya kwanza katika makosa ya
kinidhamu, kwa kipindi cha julai 2020 mapaka septemba 2021 walimu 931
walishitakiwa kwa kosa la utoro, ambao ni 51.9% ya makosa yote ‘’
Hatahivyo, ametoa wito kwa kwa walimu kuhakikisha kwamba wanajua wajibu
wao ,kanuni, taratibu zinazomamia maadilishi ya utumishi wa umma.
Mwisho.
Comments
Post a Comment