VIONGOZI WA SERIKALI WASHAURIWA KUJADILI MAMBO YANAYOHUSU NCHI NA KUACHANA NA MALUMBANO

 


Na Mwandishi wetu,Dodoma.

VIONGOZI wa serikali wameshauriwa kujadili mambo yanayohusu nchi katika vikao vyao na kuachana na mambo ambayo yanaweza kuharibu amani ya nchi.

Ushauri huo umetolewa leo jijini Dodoma na Sheikh Omary Salim wa msikiti wa Dar Mustapha Chang’ombe uliopo chang’ombe wakati akizungumza na waandishi wa habari.

Wakati huo huo,  amewataka viongozi wa dini kuacha kutumika kisiasa   watumike kiimani katika kuiombea nchi  na taifa kwa ujumla isiingie katika machafuko na kuishauri Serikali katika mambo ya kimaendeleo.

’Ningeshauri viongozi wa mihimili kuheshimiana ,nikizungumza hili nikiwa na maana moja kati ya mambo yanayoweza kuvuruga amani ya nchi ni maneno ,Maneno ndiyo ambayo yanaweza yakatupa amani katika nchi yetu na ndo yanaweza yakatupa matatizo katika nchi yetu’’

Sambamba na hayo amemuomba  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan ,katika teuzi zake kuwatazama viongozi wa dini wenye  hofu ya Mungu  kuwa wawakilishi kwenye nyadhifa mbalimbali za Serikali.

Hatahivyo , amesema katika kuukaribisha mwaka ni muhimu wananchi wakajiepusha na vitendo vya uhalifu ili waweze kuupokea mwaka kwa amani na utulivu.

 

 

Video 1

Subtitle ‘Video: 00:00:00:00 -00:00:29:04  :Jina: Sheikh Omary Salim wa msikiti wa Dar Mustapha Chang’ombe na Mkuu wa Idara ya dini Taifa vijana BAKWATA

 

Video 2

 

Subtitle ‘’watu lazima wazungumze lakini unazungumza nini? Na una uzungumza kwenye wakati upi na katika hali ipi?kwamba watu wanasema wapewe uhuru wa kuzungumza ni sahihi mtu ana uhuru wa kuzungumza shida ni kwamba ili kuilinda amani ya nchi unazungumza nini na  wakati upi na kwa mazingira yapi? ‘’ Video:00:00:29:04-00:00:55:07

 

Video 3

Subtitle ‘’Hivyo nawashauri viongozi wangu ambao mtakuwa mnasikia sauti hii ,mimi ni kiongozi wa dini na napenda kuwashaurini kuwa waadilifu na kuheshimiana hili ni suala la msingi sana ili kulinda amani ya nchi yetu .Ulimi ni silaha kubwa sana ambayo inaweza ikahifadhi nchi na inaweza ikabomoa nchi ,Mwenyezi Mungu atuhifadhi katika hayo ‘’ Video: 00:00:55:07-00:01:30:18

 

Comments

Dodoma News
Mwanza City, Mwanza, Tanzania
Dennis G. Harrison, mmiliki mwenza wa Mtandao wa Dodoma News Blog, alizaliwa mkoani Morogoro zaidi ya miaka 40 iliyopita. Dennis ana Taaluma ya Uandishi wa Habari (Proffessional Journalism) kutoka Chuo Kikuu cha Mtakatifu Augustine (SAUT). Mwaka 2009 alimaliza Shahada ya Uzamili katika Mawasiliano ya Umma, ikijikita katika Menejimenti ya Uhusiano kwa Umma na Matangazo katika chuo cha SAUT. Mwaka 2002, Dennis aliajiriwa katika Shirika la Posta Tanzania, Ofisi kuu ya Mwanza. Mwaka 2009 aliajiriwa katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Iringa kwa nafasi ya Afisa Habari. Akiwa katika ofisi hiyo alifanya kazi kwa juhudu na maarifa na kufanikiwa kuchaguliwa na wafanyakazi wote kuwa mfanya kazi bora. Kufuatia juhudi na utendaji kazi wake, alipanda hadi nafasi ya Afisa Habari Mwandamizi.