Rais Samia apongezwa



Na Rhoda Simba ,Dodoma

 

HALMASHAURI kuu ya Chama Cha Mapinduzi CCM Wilaya ya Dodoma mjini imempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan kwa uchapakazi wake ,Upendo amani , utulivu na jinsi anavyoendelea kuijenga Dodoma.

 

 Kauli hiyo imetolewa na Mwenyekiti wa Chama hicho Wilaya ya Dodoma Mjini Meja Mstaafu Johnick Risasi  kwenye kikao Cha Halmashauri kuu ya Chama ambacho hufanyika kila mwaka kwa lengo la kujadili mambo mbalimbali ya chama ikiwemo utendaji kazi.

 

Aidha Meja Risasi amesema kuwa kupitia mkutano huo wajumbe wote wameridhia kumpongeza Rais Samia Suluhu Hassan kwa jinsi ambavyo amekuwa mchapakazi  hodari katika kutekeleza Ilani ya Chama huku akiweka nchi katika amani,utulivu, mshikamano,upendo na kuwa Nchi ya kuigwa barani Afrika.

 

Amesema kuwa Rais ameendelea kuifungua Nchi kidipromasia na mataifa mengine iliyopelekea kuwepo kwa wawekezaji Wengi kuja kuwekeza na kuinua uchumi wa Taifa.

 

"Kwetu sisi kama wana Dodoma tunayo sababu nyingi za kumpongeza Rais Samia kwa namna anavyoendelea kuijenga Dodoma yetu hasa miradi mikubwa ikiwemo uwanja wa ndege ,ujenzi wa barabara ya mzunguko,uwanja wa mpira wa kisasa hali ambayo imeleta maendeleo kwa jamii ,

 

"Pia Rais wetu tunampongeza kwa Kutoa fedha bilioni 2.9 kwa ajili ya kujenga vyumba vya Madarasa zaidi ya 143 na Kutoa mwanya kwa wototo kupata elimu ya Sekondari bila wasiwasi hivyo tunapomaliza mwaka tumeona tumpongeze "amesema Risasi.

 

Katibu wa Chama hicho Wilaya ya Dodoma Sofia Kibaba akitoa maagizo kwa wajumbe kuwa ili chama kiweze kusonga mbele wanapaswa kufanya kazi kwa ushirikiano na upendo huku wakifuata maagizo ya viongozi wao.

 

Nae Mbunge wa Jimbo la Dodoma Mjini Antony Mavunde amesema kuwa wana Dodoma wana faraja kubwa hasa maendeleo yaliyopo kutokana na Rais ambaye amekuwa akionesha dhamira yake ya kutaka kuendeleza makao makuu ya nchi.

 

"Rais amekuwa wazi kuliunganisha Taifa letu bila kujali dini,ukabila itikadi zetu za vyama jambo ambalo limeendelea kuweka imani kubwa kwa wananchi "amesema Mavunde

 

Amesema kwa kushirikiana na wananchi wake atahakikisha anatekeleza zile ahadi alizozitoa wakati akiomba kura kwenye kata zote ikiwemo ujenzi wa shule , barabara ,umeme na maji.

 

Wakiongea kwa nyakati tofauti baadhi ya wajumbe wa mkutano huo Christina Kamunya pamoja na Diwani wa kata ya Mtumba Edward Maboji  wamesema kuwa kwa kipindi kifupi Rais Samia ameonesha uhodari kuleta maendeleo .

 

"Kitendo cha Rais kumwaga madarasa kila kona haijawahi kutokea hali hiyo itasaidia kuongeza muamko wa elimu hapa nchini "amesema Diwani Edward.

 

 


Comments

Dodoma News
Mwanza City, Mwanza, Tanzania
Dennis G. Harrison, mmiliki mwenza wa Mtandao wa Dodoma News Blog, alizaliwa mkoani Morogoro zaidi ya miaka 40 iliyopita. Dennis ana Taaluma ya Uandishi wa Habari (Proffessional Journalism) kutoka Chuo Kikuu cha Mtakatifu Augustine (SAUT). Mwaka 2009 alimaliza Shahada ya Uzamili katika Mawasiliano ya Umma, ikijikita katika Menejimenti ya Uhusiano kwa Umma na Matangazo katika chuo cha SAUT. Mwaka 2002, Dennis aliajiriwa katika Shirika la Posta Tanzania, Ofisi kuu ya Mwanza. Mwaka 2009 aliajiriwa katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Iringa kwa nafasi ya Afisa Habari. Akiwa katika ofisi hiyo alifanya kazi kwa juhudu na maarifa na kufanikiwa kuchaguliwa na wafanyakazi wote kuwa mfanya kazi bora. Kufuatia juhudi na utendaji kazi wake, alipanda hadi nafasi ya Afisa Habari Mwandamizi.