Na.WAMJW, DODOMA.
Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Mhe.Samia Suluhu Hassan anakusudia kuitenganisha Wizara ya Afya ili kuunda wizara mbili ili kuboresha ufanisi wa kutoa huduma kwa jamii.
Amebainisha hayo leo Tarehe 16 Desemba 2021 jijini Dodoma katika uzinduzi wa Kamati hii ya Kitaifa ya Ushauri wa Utekelezaji wa Ahadi za Nchi kuhusu Haki za Kiuchumi kwa Wanawake ambalo ni eneo muhimu katika kufikia Kizazi chenye Usawa ambapo kamati hiyo yenye wajumbe 25 kutoka sekta mbalimbali ambao wanatarajiwa kufanikisha kumuinua mwanamke kiuchumi
Mhe.Samia Amesema kuwa
takwimu zinaonyesha kuwa nusu ya watu Dunuani ni wanawake bado sehemu kubwa ya
dunia haijatoa nafasi sitahiki kuitumia ipasavyo nguvu kazi ya wanawake ambao
wakitumika vema wanauwezo mkubwa wa kuchangia uchumi wa Dunia dola za
kimarekani Tilioni 28 kwa mwaka.
" Maamzi yangu ni
kuitenga wizara itakayo shughurikia Jinsia Maendeleo ya Jamii,Jinsia,
,Wazee na Watoto kutoka
kwenye kuchanganywa na Wizara ya Afya kwa Sababu tukiweka Wizara ya afya na
hali tuliyonayo sasa Duniani Sekta ya Afya Peke yake inachukua sura kubwa ya
wizara hii kiliko vipengele vingine vilivyobaki lakini kama tutatenga vipengele
vingine ili Afya isimame peke yake usimamizi wa sera sheria na mambo mengine
unaweza kwenda vizuri kwa msukumo unaohitajika amesema Mhe.Samia Rais wa
Tanzania
Awali akitoa taarifa kwa
Mhe.Ras Samia, Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Njinsia Wazee na Watoto
Dkt.Dorothy Gwajima amesema kuwa kutokana maagizo ya mkutano wa June 8 2021
jijini Dodoma Wizara zinazoshughulikia maswala ya Jinsia upande wa Tanzabnia
Bara na Zanzibar ilianza kulifanyia kazi agizo kwa kuhakikisha kuwa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania inatimiza ahadi yake ya kuwa kinara katika eneo la
haki na usawa wa kiuchumi nchini ambapo wanawake na wanaume watakuwa na fursa
na haki sawa katika kunufaika na uwezeshaji kiuchumi. Pamoja na kuzindua Kamati
hii leo, Wizara pia imeweza kuratibu uandaliwaji wa Mpangokazi
Jumuishi na Shirikishi wa Taifa.
Comments
Post a Comment