Na Rhoda Simba, Dodoma.
WAZIRI wa Katiba na Sheria
Prof. Palamagamba Kabudi anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika mkesha wa mwaka
mpya kwa niaba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu
Hassan,Mkesha wa kuliombea taifa pamoja na viongozi mbalimbali.
Hayo yamesemwa leo Disemba
29 jijini hapa na Askofu Mkuu wa kanisa la Tanzania Fellowship of Churches Dk
Godfrey Malassy na Mwenyekiti wa kamati ya maandalizi ya mkesha mkubwa wa
mwaka mpya ambapo amesema kuwa mkesha huo unalenga kuliombea taifa.
Amesema katika mkesha huo ambao
utafanyika katika uwanja wa Jamhuri kuamkia mwaka Mpya wa 2022 Rais amemtuma
Waziri wa Katiba na Sheria Prof Palamagamba Kabudi kuwa mgeni rasimi kwa niaba
yake.
Dk Mallasy amesema kuwa nchi ya
Tanzania inatakiwa kuendelea kuwa na amani,upendo na ushirikiano wa kweli.
Aidha amesema kuwa mkesha huo
utahakikisha unafanya maombi kwa ajili ya kuliombea taifa kutoingia katika
machafuko pamoja na watumishi wa umma.
"Tumekuwa tukishuhudia
machafuko yakitokea katika mataifa mbalimbali na machafuko haya
yanasababishwaa kukosekana kwa amani na kudhoofika kwa uchumi.
"Watanzania tunatakiwa
kulinda sana amani na kuhakikisha upendo unaendelea kati ya mtu na mtu pamoja
na jamii kwa ujumla wake"amesema Mallasy.
Mwisho.
Comments
Post a Comment