Na Rhoda Simba,Dodoma.
MKUU wa Mkoa wa Dodoma Antony
Mtaka ameuagiza uongozi wa Ofisi ya Mkurugenzi wa jiji na Afisa Elimu
kuhakikisha wanasambaza walimu wa sekondari katika shule zenye uhaba
badala ya kuacha walimu kurundikana shule moja.
Aidha amesema zipo shule za
sekondari ndani ya jiji ambazo zina walimu wengi na zilizopo
pembezoni mwa jiji zina walimu wachache, kutokana na hali hiyo
Ofisi ya afisa elimu na Ofisi ya Mkurugenzi wa jiji waone namna ya
kuweza kuwasambaza walimu waliokuwa wengi katika shule za pembezoni
ambazo zina uhaba.
Mtaka ameyasema hayo Disemba
22 jijini hapa wakati wa ziara ya ukaguzi wa ujenzi wa vyumba vya
madarasa katika shule za sekondari zilizojengwa kwa fedha za mkopo wa mashart
nafuu unaotokana na mapambano dhidi ya uviko 19.
Amesema Mkoa wa Dodoma ni
kati ya mikoa ambayo imefanikiwa kufanya ujenzi wa vyumba bora vya
madarasa ambayo yana ubora wa kiwango cha juu
"Dodoma tumeweza kujenga
madarasa yenye ubora unaoendana na thamani ya fedha lakini napenda kutoa
maagizo katika Ofisi ya Mkurugenzi na afisa elimu kukutana mkaona ni
namna gani ya kufanya utaratibu wa kupunguza
walimu waliozidi
katika baadhi ya shule na kuwapeleka katika shule ambazo zina uhaba wa walimu,
"Na jambo hili liwekwe wazi
kwa walimu kuwa ni kwa nia njema ili kuifanya elimu ya wanafunzi wa jiji
la Dodoma kuwa bora zaidi na ilingane na viwango vya ubora wa
madarasa" amesema Mtaka
Hata hivyo ametoa maelekezo kwa
Ofisi ya Mkurugenzi wa jiji la Dodoma na Ofisi ya afisa elimu wa jiji kutoa
taarifa kwa wakuu wote wa shule kuwa pindi shule zitakapofunguliwa
tarehe 17 January 2022 kila mwanafunzi awajibike kupanda miti na
kuuutunza.
Nae Mkurugenzi wa jiji Joseph
Mafuru amesema ujenzi huo unatarajia kabla ya sikukuu ya chris mass utakuwa
umekamilka na funguo zitakabidhiwa tayari kwaajili ya maandalizi ya
wanafunzi kuanza masomo.
Mwishoo.
Comments
Post a Comment