Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam
*Mhe. Amos Makalla* amewaelekeza *TARURA* kuhakikisha wanashirikiana na *Baraza
la Madiwani* katika kuchagua *Barabara za kipaumbele* Cha Ujenzi na sio
*kujiamulia hao wenyewe.*
*RC Makalla* ametoa maelekezo
hayo wakati wa ufunguzi wa kikao Cha *bodi ya Barabara* ambapo amesema
*Madiwani Kama wawakilishi wa Wananchi ndio wanaelewa Barabara zenye changamoto*
kubwa na zinazotegemewa na Wananchi wengi hivyo *Ni muhimu wakashirikishwa.*
Aidha *RC Makalla* amewaelekeza
*TARURA na TANROAD* kuhakikisha *wanalinda Miundombinu ya Barabara* zao
hususani maeneo ya *watembea kwa miguu yasivamiwe upya* na Wafanyabiashara.
Hata hivyo *RC Makalla*
amewataka *Wakandarasi* wanaotekeleza Miradi ya Barabara *kukamilisha Ujenzi
kwa wakati* na kushirikiana na Wananchi na *Serikali ya Mtaa wa eneo husika ili
wajue Nini kinaendelea katika mtaa wao.*
Pamoja na hayo *RC Makalla*
ametaka *TANROAD, TARURA na Wakandarasi* kuenda sambamba na *maono ya Rais
Samia Suluhu Hassan* katika kuwafikishia Wananchi Maendeleo kwa wakati.
Comments
Post a Comment