Na. Dennis Gondwe, DODOMA
Mstahiki
Meya wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma, Prof. Davis Mwamfupe amewatakia heri ya Mwaka
mpya 2022 madiwani na wafanyakazi wa halmashauri hiyo na kuwaombea afya njema.
Meya, Prof. Davis Mwamfupe |
Akitoa
salaam za Mwaka mpya 2022 ofisini kwake, Prof. Mwamfupe alisema kuwa anawaombea
afya njema kwa Mwaka 2022 ili waweze kutekeleza majukumu yao.
“Waheshimiwa
madiwani na wafanyakazi wote, niwaletee salaam za kuwatakia Mwaka mpya wa 2022.
Nikiwa na matumaini kuwa kwa rehema zake Mungu tutavuka salama. Leo
tunasherehekea karibu kumaliza mwaka wa 2021. Matukio yote haya mawili yanabeba
ujumbe mkuu kuwa tunaposherehekea kumaliza Mwaka 2021 haimaanishi kuwa
tumeyashinda na kuyatimiza yote tuliyoyapanga, la hasha, tunasherehekea kwa
sababu pamoja na changamoto zote bado tumedumu kama taasisi. Vilevile,
tunasherehekea kwa sababu tunaamini kuwa Mungu anatupa fursa nyingine ya kupanga
yajayo. Tusipokuwa na matumaini ya mazuri yajayo hatuwezi kuwa na furaha”
alisema Prof. Mwamfupe.
Aidha,
aliwatakakusameheana na kusahau yaliyopita ili kuanza mwaka mpya wakiwa wamoja.
“Sasa basi, hebu tusafishe mioyo yetu kwa kusameheana tulipokwazana. Ni pale tu
mioyo yetu ikiwa safi ndipo Mungu hutupa matumaini ya kupanga yajayo. Nawatakia
wote na familia zenu siku kuu njema ya Mwaka mpya 2022” alisema Prof. Mwamfupe.
Akiongelea
matarajio ya Mwaka mpya 2022, alisema kuwa wanatakiwa kujipanga vizuri zaidi
katika kutoa huduma kwa wananchi wa Jiji la Dodoma na kuwaletea maendeleo.
MWISHO
Comments
Post a Comment