JESHI LA POLISI DODOMA KWA KUSHIRIKIANA NA IDARA YA UHAMIAJI YAKAMATA WAHAMIAJI HARAMU 51

 


Na Rhoda Simba, Dodoma.

JESHI la polisi Mkoani Dodoma limewatia mbaroni wahamiaji haramu 51 raia wa Ethiopia na watu wawili raia wa Tanzania waliokuwa wakisafirishwa katika gari la mizigo wakitokea kanda ya kaskazini kuelekea Mikoa ya Kusini.

 

Akizungumza na vyombo vya habari  leo Disemba 28 jijini hapa kamanda wa Polisi Mkoa
wa Dodoma SACP Onesmo Lyanga amesema kuwa watuhumiwa hao wamekamatwa tarafa ya Bereko Wilaya ya Kondoa wakiwa kwenye gari lenye namba za usajili T.593 AUE aina ya fuso likiendeshwa na Ignas Mgosi (23) mkazi wa mafinga akisaidiwa na Jafari Idd (39) mkazi wa Arusha.

 

 

“Askari walipekua gari  hilo  na kuwakamata wahamiaji hao raia wa Ethiopia wakitoa moshi kilimanjaroi kwenda iringaa mbinu iliyotumika ni kuwaficha kwa turubai kiinji cha  tukio ni kukosa uzalendo wa nchi na tamaa mbaya ya mkujiptia kiipato  isivyo halali” amesema  kamanda Lyanga.

 

 

 

Aidha ametoa wito kwa vijana wa kitanzania na madereva na wamiliki wa magari kuwa waache tamaa ya kufanya vitendo vya uhalifu kwa kuwa uhalifu haulipi.

 

 “Kwa mujibu wa sheria ya nchi  kifungu 46 (1) (a) – (g) cha sheria ya uhamiaji sura  ya 54 siyo tu watuhumiwa kufikishwa  mahakamani na kupata hukumu ya kifungo bali ni pamoja na gari lililohusika kufirisiwa na wamiliki kupata umasikini”amesema  Lyanga

 

Kwa upande wake Mrakibu Mwandamizi wa Uhamiaji Mkoa wa Dodoma ambaye pia ni kaimu Afisa uhamiaji  Adam Mkuyu amesema wamejipanga kila kona kuhakikisha hakuna mhamiaji anaingia kinyemela.

 

“Sisi uhamiaji tumejipanga kila sehemu kuhakikisha  vitendo hivi vya uhamiaji haramu  tunavipiga vita vikali lakini pia nitoe wito kwa wenzetu ambao wanahitaji kuhamia nchini kwetu wafate sheria na kanuni za uhamiaji”amesema Mkuyu.

Comments

Dodoma News
Mwanza City, Mwanza, Tanzania
Dennis G. Harrison, mmiliki mwenza wa Mtandao wa Dodoma News Blog, alizaliwa mkoani Morogoro zaidi ya miaka 40 iliyopita. Dennis ana Taaluma ya Uandishi wa Habari (Proffessional Journalism) kutoka Chuo Kikuu cha Mtakatifu Augustine (SAUT). Mwaka 2009 alimaliza Shahada ya Uzamili katika Mawasiliano ya Umma, ikijikita katika Menejimenti ya Uhusiano kwa Umma na Matangazo katika chuo cha SAUT. Mwaka 2002, Dennis aliajiriwa katika Shirika la Posta Tanzania, Ofisi kuu ya Mwanza. Mwaka 2009 aliajiriwa katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Iringa kwa nafasi ya Afisa Habari. Akiwa katika ofisi hiyo alifanya kazi kwa juhudu na maarifa na kufanikiwa kuchaguliwa na wafanyakazi wote kuwa mfanya kazi bora. Kufuatia juhudi na utendaji kazi wake, alipanda hadi nafasi ya Afisa Habari Mwandamizi.