WAZIRI MAJALIWA KUWA MGENI RASMI KWENYE SHEREHE ZA KITAIFA ZA UZINDUZI WA MAADHIMISHO YA MIAKA 60 YA UHURU
DODOMA
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kasim Majaliwa
anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika sherehe za kitaifa za uzinduzi wa maadhimisho ya miakia 60 ya uhuru Tanzania
Bara, yatakayo fanyika Disemba 2 katika mji wa serikali mtumba uliopo Mkoani
Dodoma.
Akizungumza na Waandishi wa Habari leo, MKuu wa Mkoa Antony
Mtaka, amesema sherehe za uzinduzi zitaanza saa 12: 30 asubuhi zikiambatana na
shughuli mbalimbali ikiwemo uzinduzi wa ujenzi wa ofisi za Wizara awamu ya pili
zinazojengwa katika Mji wa Serikali Mtumba.
‘’Uzinduzi wa huduma za kijamii katika Mji wa Serikali Mtumba
ikiwa ni pamoja na uwekaji wa jiwe la
msingi la kituo cha polisi chenye hadhi ya daraja la kwanza,ukaguzi wa barabara
za lami za Mji wa serikali Mtumba zenye jumla ya km 51.2 ambazo ujenzi wake umefikia
zaidi ya 85% na ukaguzi wa jengo la kitega uchumi la Halmashauri ya Jiji la
Dodoma lilipo katika Mji wa Serikali Mtumba’’
Aidha, Mtaka amesema serikali kwa kutambua umuhimu wa miaka
60 ya uhuru, ilitoa maelekezo na mwongozo wa kufanyika kwa shughuli mbalimbali
za maendeleo ,uchumi na biashara ,michezo na kijamii kama sehemu ya sherehe za
maadhimisho kuanzia novemba 1,2021 hadi itakapohitimishwa Disemba 9 ,2021
jijini Dar es salaam.
Mtaka ametumia fursa hiyo, kutoa wito kwa taasisi za
serikali, binafsi, makundi mbalimbali na wananchi wote wa Dodoma na Mikoa
jirani kujitokeza kwa wiki katika sherehe hizo.
‘’katika kurahisisha usafiri wa wananchi kwenda kwenye eneo
la Mji wa Serikali Mtumba kwaajili ya tukio hili pamoja na maandalizi ya
usafiri yaliyofanywa na kamati ya maandalizi,niwaagize Jeshi la Polisi (Usalama
Barabarani) Mkoa wa Dodoma,kuruhusu daladala za kubeba abiria kutoka viunga
mbalimbali vya Jiji la Dodoma kupeleka na kuchukua abiria kwenye eneo la Mji wa
Serikali Mtumba’’
Maadhimisho haya , yanakwenda sambamba na kauli mbiu isemayo ‘’
Miaka 60 ya Uhuru Tanzania Imara kazi iendelee’’
Mwisho
Comments
Post a Comment