Kaimu Mkurugenzi Idara ya Miliki TBA,Bw.Said Mndeme,akizungumza na Katibu Mkuu wa Wizara ya Ardhi na Maendeleo ya Makazi Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ),Joseph Kilangi pamoja na watumishi wa Wakala wa Majengo Zanzibar (ZBA) ambao walifanya ziara ya kujifunza na kujionea miradi mbalimbali ambayo inatekelezwa na TBA Jijini Dodoma.
Kaimu Mkurugenzi wa Wakala wa Majengo Zanzibar (ZBA) Mhandisi Kassim Omar,akielezea jambo wakati wa ya kujifunza na kujionea miradi mbalimbali ambayo inatekelezwa na TBA Jijini Dodoma.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Ardhi na Maendeleo ya Makazi Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ),Joseph Kilangi (aliyevaa miwani) akimsikiliza Mhandisi ujenzi katika eneo la Viwanda vya Tofali na Zege Athu Chulla akitoa maelezo ya mradi katika eneo la Nzuguni wakati wa ziara ya kujifunza na kujionea miradi mbalimbali ambayo inatekelezwa na TBA Jijini Dodoma.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Ardhi na Maendeleo ya Makazi Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ),Joseph Kilangi (aliyevaa miwani) akifafanua jambo wakati wa ziara ya kujifunza na kujionea miradi mbalimbali ambayo inatekelezwa na TBA Jijini Dodoma.
Mratibu wa ujenzi wa nyumba 3,500 Nzugani Dodoma (Awamu ya kwanza nyumba 150) Fedrick Jackson,akimpa maelezo Katibu Mkuu wa Wizara ya Ardhi na Maendeleo ya Makazi Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ),Joseph Kilangi (aliyevaa miwani) pamoja watumishi wa wakala wa majengo Zanzibar (ZBA) wakati wa ziara ya kujifunza na kujionea miradi mbalimbali ambayo inatekelezwa na TBA Jijini Dodoma.
Ujenzi wa nyumba 150 katika eneo la Nzuguni ukiendelea
Katibu Mkuu wa Wizara ya Ardhi na Maendeleo ya Makazi Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ),Joseph Kilangi akiangalia ujenzi wa mradi katika Mji wa Kiserikali Mtumba wakati wa ziara ya kujifunza na kujionea miradi mbalimbali ambayo inatekelezwa na TBA Jijini Dodoma.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Ardhi na Maendeleo ya Makazi Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ),Joseph Kilangi,(aliyevaa miwani) akitoa maelezo mara baada ya kukagua ujenzi wa nyumba 20 zilizopo katika eneo la Kisasa wakati wa ziara ya kujifunza na kujionea miradi mbalimbali ambayo inatekelezwa na TBA Jijini Dodoma.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Ardhi na Maendeleo ya Makazi Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ),Joseph Kilangi ,akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kufanya ziara ya kukagua,kujifunza na kujionea miradi mbalimbali ambayo inatekelezwa na TBA Jijini Dodoma.
Kaimu Mkurugenzi Idara ya Miliki TBA,Bw.Said Mndeme,akimpongeza Katibu Mkuu wa Wizara ya Ardhi na Maendeleo ya Makazi Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ),Joseph Kilangi kwa kutembelea miradi mbalimbali ambayo inatekelezwa na TBA Jijini Dodoma.
Kaimu Mkurugenzi wa Wakala wa Majengo Zanzibar (ZBA) Mhandisi Kassim Omar,akielezea jinsi walivyojifunza katika ziara ya kukagua miradi mbalimbali ambayo inatekelezwa na TBA Jijini Dodoma.
Mkurugenzi Idara ya ujenzi TBA,Mhandisi Likimaitare Naunga,akiwaahidi ushirikiano viongozi wa ZBA katika kutekeleza miradi mbalimbali nchini pamoja na kubadilishana uzoefu wa kazi.
Dodoma
Katibu
Mkuu wa Wizara ya Ardhi na Maendeleo ya Makazi Serikali ya Mapinduzi ya
Zanzibar (SMZ),Joseph Kilangi amesema mpango uliopo kwa sasa ni Wakala wa
Majengo Tanzania (TBA) kushirikiana na Wakala wa Majengo Zanzibar (ZBA) katika
kutekeleza miradi mbalimbali visiwani Zanzibar.
Pia
wameridhishwa na miradi inayotekelezwa na Wakala wa Majengo Tanzania (TBA)
ambapo kupitia Wakala wa Majengo Zanzibar (ZBA) wameahidi kufanya miradi yenye
kiwango kama hicho visiwani Zanzibar.
Kauli
hiyo ameitoa Novemba 26,2021 wakati wa ziara ya Wakala wa Majengo Zanzibar
(ZBA) kujifunza na kujionea miradi mbalimbali ambayo inatekelezwa na TBA Jijini
Dodoma.
Miradi
hiyo ni pamoja na ule wa Mji wa Kiserikali Mtumba awamu ya pili,mradi wa ujenzi
wa nyumba 3500 wa watumishi wa umma,Nzuguni ambao umeanza na nyumba 150 na
mradi wa ujenzi wa nyumba 20 za viongozi katika eneo la Kisasa.
Katibu
Mkuu Kilangi amesema kwa sasa wanaiamini TBA kwa asilimia mia moja hivyo
watashirikiana na ZBA kutekeleza miradi mbalimbali visiwani Zanzibar kwa lengo
la kupata miradi yenye ubora kama Tanzania Bara.
“Sasa
mimi nadhani tuiamini TBA kwa asilimia miamoja kama tunamiradi tutakayoianzisha
basi TBA na wana miradi Zanzibar tutawaleta wataalamu wetu waje wafanye kazi
kwa pamoja na TBA.
“Wanzanzibar
wategemee tutawaalika TBA Zanzibar, wategemee mambo mazuri hizi fedha
tulizopata tuna bilioni 460 zinaenda mifukoni mwa watu kupitia miradi
mbalimbali.Tutawambia waje Zazibar wasimamie miradi yetu,”amesema.
Aidha,amesema
mradi wa Mji wa Serikali awamu ya pili ni mzuri na utaonesha kwamba Dodoma ni
Makao Makuu ya Serikali kama ilivyo Lagos na ndoto ya Hayati mwalimu Julius
Kambarage Nyerere itakuwa imetimia kwa vitendo.
“Mradi
ule wa Mji wa Serikali ni mzuri sana na majengo yale hasa awamu ya pili
ikikamilika mji utakuwa ni mzuri sana lakini itaonesha kwamba hapa ni Makao
Mkuu ya Nchi hata ukienda Lagos utaona hili nadhani ile ndoto ya Baba wa Taifa
itatimia.
“TBA
wamekuja na michoro mizuri na inajengwa kileo sana mazingira ni mazuri na
vitendea kazi vimezingatia ubora,baada ya miaka miwili mitatu itaonekana kweli
ni makao makuu ya Serikali,”amesema.
Kuhusiana
na nyumba za watumishi wa umma zinazojengwa na TBA, amesema mradi huo utakuwa
na manufaa makubwa kwani watumishi wataweza kukaa katika nyumba nzuri.
Hata hivyo
ameipongeza TBA kwa kufanya kazi nzuri ikiwa ni pamoja na kuwa na vifaa pamoja
na wataalamu wa kutosha.
“Mimi
kwa TBA kwakweli kwa uwezo nilioouna mimi nadhani hata kama kuna wakandarasi
wengine kuna miradi mbalimbali ya ujenzi ni kushawishi tu waitumie TBA kama ni
Mkandarasi waitumie TBA kama ni msimamizi kwa sababu wana uwezo wote wana vifaa
wana zana na wana wataalamu wa kutosha,”amesema.
Kwa
upande wake,Kaimu Mkurugenzi wa Wakala wa Majengo Zanzibar (ZBA) Mhandisi
Kassim Omar amesema lengo la ziara hiyo ni kujifunza yale ambayo TBA
wanayafanya ambapo kwa kiwango kikubwa yanalingana na majukumu ya ZBA.
''Zanzibar
kwa sasa wapo katika matayarisho ya Mji wa Kiserikali visiwani humo ambapo
utekelezaji wao utakuwa ni mkubwa ambapo amewakaribisha TBA waone yale ambayo
wameyaonesha tutakavyoyatekeleza.''amesema Mhandisi Omar
Naye,Kaimu
Mkurugenzi Idara ya Miliki TBA,Bw.Said Mndeme amesema ziara hiyo imekuwa na
manufaa makubwa kwani ZBA wameweza kuona mradi wa nyumba za watumishi wa umma
na wameona jinsi walivyoutekeleza mradi huo na wameweza kujionea jinsi ambavyo
wamejipanga katika eneo la material pamoja na viwanda mbalimbali ambavyo
wamevianzisha.
Kwa
upande wake Mkurugenzi Idara ya ujenzi TBA,Mhandisi Likimaitare Naunga
ameishukuru ZBA kwa kuichagua TBA kama sehemu ya kupata uzoefu katika sekta ya
ujenzi ambapo amedai wapo tayari kwa ajili ya ushirikiano huo.
Comments
Post a Comment