Na Rhoda Simba ,Dodoma.
KUELEKEA mashindano ya Mabunge ya Afrika Mashariki hii leo, klabu ya michezo ya Bunge imepokea vifaa vya michezo kutoka sports pesa ikiwa ni moja ya maandalizi kuelekea mashindano hayo yanayo tarajiwa kupigwa mwezi ujao jijini Arusha
Akizungumza na waandishi wa habari Bungeni jijini hapa Mwenyekiti wa klabu ya bunge na mwenyekiti wa Bodi ya wakurugenzi kutoka sports pesa ambaye pia ni mbunge wa kinondoni mheshimiwa Abas Tarimba amesema maandalizi waliyo yafanya msimu huu ni makubwa hivyo wanatarajia kufanya vizuri kwenye mashindano hayo.
“Napenda kuuthibitishia Umma
kwamba sisi kama timu ya bunge tumejiandaa vizuri na tunahakikisha kuwa
tutashinda mashindano hayo, michezo ambayo tutashiriki ni pamoja na football
kwa wanaume kuna netball kwa wanawake riadha,vollebay pamoja na kuvuta kamba
hivyo bunge la Tanzania linatayarishwa katika msafara mzito wa watu 100,
“Tumekuwepo Dodoma toka tarehe
21 kwaajili ya mazoezi na jana tulifanya kikao cha kutathimini namna michezo
yetu itavyofanyikka na kutokana na matayarisho yetu hakika tunaenda kuchukua
ushindi amesema Tarimba.
Aidha amsema timu zipo vizuri na
hakuna majeruhi na kikubwa wanaomba taasisi nyingine ziweze kuwasaidia kutoa
morali kwa wachezaji kama ilivyo kampuni ya sportpesa ambavyo imekuwa ikitoa
vifaa vya michezo.
Kwa upande wake Kaimu katibu wa
bunge Mohamed Mwanga mara baada ya kupokea vifaa hivyo vya michezo ameupongeza
uongozi wa sports pesa Huku akiwataka wachezaji wote wa bunge kujitoa na
kuhakikisha wanatakiwa washindi wa ujumla kwenye mashindano
Hata hivyo Timu mbalimbali za mabunge ya Afrika mashariki
zinatarajiwa kushirIki mashindano hayo Jijini Arusha Disemba mwaka huu.
MWISHO.
Comments
Post a Comment