Na Munir
Shemweta, WANMM MOROGORO
Naibu
Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula amekitaka
Chuo cha Ardhi Morogoro (ARIMO) kujipanga na kuhakikisha kinamaliza kazi ya
urasimishaji makazi katika maeneo waliyopewa kazi hiyo.
Hatua
hiyo inafuatia Naibu Waziri Dkt Mabula kuelezwa na Mkuu wa Chuo cha ARIMO
Huruma Lugalla kuwa, moja ya changamoto kubwa katika zoezi zima la
urasimishaji makazi maeneo mbalimbali ambayo chuo hicho imechukua kazi hiyo ni
kasi ndogo ya uchangiaji gharama kutoka kwa wananchi.
‘’Mhe.
Naibu Waziri uchangiaji katika zoezi la urasimishaji makazi katika maeneo
mbalimbali nchini tunayoyafanyia kazi hasa hapa Morogoro ni mdogo sana pamoja
na gharama ya zoezi hilo kupungua kutoka shilingi 150,000 hadi 130,000/=’’
alisema Lugala
Hata
hivyo, pamoja na kuelezwa changamoto, hiyo Dkt Mabula ambaye alikuwa
akizungumza na Uongozi wa Chuo cha Ardhi Morogoro tarehe 29 Novemba 2021,
alikitaka chuo hicho kuhakikisha kinachukua maeneo machache ya kuyafanyia kazi
badala ya kuchukua maeneo mengi aliyoyaeleza kuwa yanaweza kuwashinda
kukamilisha kazi kwa wakati.
‘’
Ni vizuri mkajipanga katika zoezi zima la urasimishaji, baada ya kufanyika kosa
la awali nyuma sasa msirudie tena kosa maana haitaleta picha nzuri kwa chuo na
mnachotakiwa ni kujipanga na kuwa na mkakati wa kukamilisha kazi’’ alisema Dkt
Mabula
Mkuu
wa koa wa Morogolo Martine Shigela alishangazwa na maelezo kuwa, baadhi ya
wananchi katika mkoa wake wanakuwa wazito kuchangia gharama za urasimishaji
makazi holela wakati wanaweza kujenga nyumba ya milioni 20 huku akishindwa
kuchangia shilingi 130,000/
‘’Yaani
wananchi wanashindwa kuchangia gharama za urasimishaji wakati wanajenga nyumba
kwa gharama kubwa kama milioni 10 mpaka 20? Hii haina afya kabisa’’alisema
Shughela.
Awali
Mkuu wa Chuo cha Ardhi Morogoro Huruma Lugalla alimueleza Naibu Waziri Dkt
Mabula kuwa Chuo chake kinaendelea na utekelezaji miradi ya urasimishaji makazi
katika mitaa 61 nchini kwa kushirikiana na halamashauri na wananchi wanaomiliki
ardhi ya makazi yaliyoendelezwa kiholela.
Kwa
mujibu wa Lugalla, jumla ya viwanja 30,188 vimeidhinishwa kufanyiwa kazi ya
urasimishaji makazi, iwanja 129, 761 vimetambuliwa huku michoro 218
ikisanifiwa na takriban Shilingi Bilioni 2.553 ikiwa imetolewa kwa ajili
ya utekelezaji wa zoezi hilo.
Aidha,
Mkuu huyo wa Chuo cha ARIMO aliwasilisha ombi la chuo chake kutaka kusaidiwa
uendelezaji eneo la ekari 33 lililoko Mlimakola Manispaa ya Morogoro kwa ajili
ya kupanua wigo wa mafunzo, miundombinu sambamba na kuongeza udahili wa
wanafunzi.
Kufuatia
ombi hilo, Mkuu wa mkoa wa Morogoro Martine Shigela alisema, ni vyema taasisi
za umma zinapoomba msaada wa uendelezaji maeneo yake zikafikiriwa kusaidiwa na
kuongeza kuwa, mkoa wake uko tayari kusaidia pale utakapoona mipango ya chuo kuhusu
uendelezaji eneo hilo.
Katika hatua nyingine Mkuu wa mkoa wa Morogoro
Martine Shighela alilitaka Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) kufikiria namna ya
kuwekeza miradi katika mkoa huo ukiwemo ule wa eneo la maduka (MALL) kwa lengo
la kurahisisha upatikanani huduma.
Akizungumza
na Menijementi ya NHC iliyomtembelea ofisini kwake wakati wa kikao chake na
Jukwaa la Wahariri Tanzania mkoani Morogoro kilichofunguliwa na Naibu Waziri wa
Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula, Shighela alisema, kwa
sasa mkoa huo hauna maduka (Mall) kwa ajili ya kuwaewezesha wananchi wa mkoa
huo kupata huduma eneo moja kama ilivyo Dar es Salaam wakati mkoa huo
unaendelea unapanuka.
Mkurugenzi
Mkuu wa Shirika la Numba la Taifa Dkt Maulid Banyani alimhakikishia Mkuu wa
Mkoa wa Morogoro kulifanyia kazi suala hilo na katika kuhakikisha utekelezaji
unafanyika haraka Shigela na timu ya NHC walitembelea eneo la Kingo Sabasaba
katika manispaa ya Morogoro kuona namna ya kufanya uwekezaji kwenye eneo
hilo.
Comments
Post a Comment