DODOMA.
Waziri wa Maji Mh. Jumaa Aweso amewagiza
watendaji wa Wizara ya Maji, Wakala wa Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini
RUWASA, Mamlaka za Maji na Usafi wa Mazingira pamoja na Bodi za Maji za Mabonde
kuhakikisha wanatumia fedha zilizotolewa kwaajili ya utekelezaji wa Mpango wa
Maendeleo kwa Ustawi wa Taifa na Mapambano dhidi ya UVIKO-19 kwa lengo lililo
kusudiwa ili kuleta manufaa kwa Taifa.
Akizungumza jijini Dodoma jana kuhusu
utekelezaji wa fedha hizo kwenye miradi ya sekta ya maji ambayo imepangiwa
kiasi cha shilingi bilioni 139.4 sawa na 10.6, Waziri Aweso amesema ,Wizara
itafuatilia kwa karibu utekelezaji wa mipango hiyo na kwa yeyote atakayezembea
na kutumia vibaya fedha hizo atachukuliwa hatua za kisheria.
‘’UVIKO-19 ituzindue kutekeleza
wajibu wetu wa kufanya kazi kwa bidii, maarifa, ubunifu, uadilifu na uzalendo
wa hali ya juu kwa kuwa maji ni hitaji la msingi hata katika mapambano ya janga
hili’’
Waziri Aweso amesema, Fedha hizo
zimeelekezwa katika maeneo ambayo yatawezesha upatikanaji wa huduma ya maji kwa
wakati na kuwa na huduma iliyo endelevu.
Amebainisha maeneo hayo yakiwa ni miradi ya kuboresha upatikanaji wa maji ambayo
itagharimu kiasi cha shilingi bilioni 104,240,738,460.00 zikiwa zimepangwa kwa
kuhakikisha angalau kila jimbo linatekelezewa mradi uliogharimu wastani wa
shilingi milioni 500. ‘’Utekelezaji wa miradi hiyo unatarajiwa kuwezesha upatikanaji
wa huduma kwa wananchi wapatao milioni2’’
Hatahivyo, amesema maeneo mengine
yakiwa ni ununuzi wa seti 25 za mitambo ya kuchimba visima vya maji ambayo
imegharimu kiasi cha shilingi bilioni 17,500,000,000.00 pamoja na ununuzi wa
mitambo ya ujenzi wa mabwawa na vifaa vya utafiti wa maji chini ya ardhi ambayo
imegharimu shilingi bilioni 17,613,835,330.00
Comments
Post a Comment