Na Mwandishi Wetu, Dodoma.
Waziri wa Maji Mh. Jumaa Aweso amewataka watendaji wa sekta
ya maji hapa nchini kwenda kutekeleza
miradi ya maji kwa uaminifu, uadilifu ,ubora na gharama zake kuwa halisia
kulingana na fedha zilizotolewa katika utekelezaji wa miradi hiyo.
Ikumbukwe kuwa Wizara ya Maji imepewa kiasi cha shilingi kiasi
cha bilioni 139.4 sawa na asilimia 10.6 kutekeleza miradi ya maji katika fedha
zilizotolewa kwaajili ya utekelezaji wa Mpango wa Maendeleo kwa Ustawi wa Taifa
na Mapambano dhidi ya UVIKO-19. Trilioni 1.3.
Akizungumza leo katika kikao cha Watendaji hao Waziri Aweso
amesema ni muhimu wakaitekeleza miradi hiyo kwa uadilifu na uamifu mkubwa.
‘’Tumepewa miezi tisa miradi hii ikamilike ,lakini sisi
tukatekeleze ndani ya miezi saba, twendeni tukajipange kuhakikisha watu
wanapata huduma ya maji , yawezekana ukawa muda mfupi kwa jeshi hili, hii kazi
tunaiweza, twendeni tukafanye kazi hii kwa kushirikiana,tunauwezo wa kuifanya
kazi hii mara moja na watu wakapata huduma ya maji’’
Aidha, Waziri Aweso amesema hana mashaka na watalaamu wake
hivyo ni matumani yake kuwa miradi hiyo itakamilika kwa muda uliokusudiwa.
‘’Sisi pesa tunazo tumeshapewa, twendeni tukafanya kazi, niwaombe
nawapa ushauri wa bure , unaweza kukosa COVID-19 ukapata fedha za COVID-19 ,hizi
fedha za COVID-19 hazilambwi, tumekutana hapa tunaelekezana ni aibu kubwa Mhandisi
unakuja kufukuzwa kizembe eti umechukua fedha kiasi fulani’’
Kwa upande wake Naibu Waziri Wizara ya Maji, Mhandisi Marryprisca
Mahundi amewataka watendaji hao kwenda kukamilisha miradi hiyo kwa wakati. ‘’Hata
uwe mtandaji mzuri vipi kama huna nidhamu kwa mwenzio unaweza kupoteza maana,
naomba mheshimiane''
Naye Katibu Mkuu Wizara ya Maji Mhandisi Antony Sanga emesema
lengo la kikao hicho ni maelekezo mahususi juu ya utekelezaji ra miradi ya maji
kupitia fedha za UVIKO-19 trilioni 1.3 .
‘’Ni lazima mkayazingatie maelekezo yale ambayo mmepatiwa, Suala
la maji halikuwepo katika fedha hizi, kwa upendo wa Rais kwa wananchi hasa katika
suala la upatikanaji wa maji safi na
salama mijini na vijini, alielekeza fedha hizo zikakabiliane na changamoto za
miradi ya maji, tumepatiwa bilioni 139.4 sawa na asilimia 10.6 zimeelekezwa
wizara ya maji’’
Mhandisi Sanga amesema kama watendaji kazi yao ni kutafsiri
kwa vitendo maelekezo ambayo Waziri ameyatoa
‘’Tukasema lazima tuitane wote watekelezaji wa miradi na kuwapa maelekezo na
msije mkakosea, sababu ni hatari kubwa kutumia pesa hizi tofauti na maelekezo
ambayo mmepatiwa, tumepanga kutekeelza miradi takribani miradi 218 na
imeelekezwa mijini na vijini’’
Hatahivyo, Katibu huyo amewataka watendaji hao kuhakikisha kuwa pindi
wanapotekeleza miradi wanakuwa na jalada au faili kuanzia hatua za mwanzo ili iwe
rahisi kufanya ufutaliliajij ‘’Lazima kuwe na ushirikishaji katika maeneo
husika, viongozi wapate kufahamu miradi inayoendelea katika utekeelezaji wa
miradi hiyo ,isitokee kiongozi akaomba taarifa mkashindwa kutoa taarifa kila
mmoja anapaswa kuzingatia hili’’
Mwisho.
Comments
Post a Comment