VIONGOZI WA SKIMU ZA UMWAGILIAJI WATAKIWA KUSIMAMIA UKUSANYAJI WA ADA NA TOZO.

 

Mhandisi Umwagiliaji Mkoa wa Iringa Bw. Onesmo Kahoggo akingumza kuhusu Viongozi wa skimu za kilimo cha Umwagiliaji Nchini, kusimamia ukusanyaji wa ada na Tozo za Umwagiliaji.

Mhandisi wa Umwagiliaji Mkoa wa Iringa Onesmo Kahongo  amewataka viongozi katika Skimu za Umwagiliaji  kusimamia kikamilifu zoezi la ukusanyaji ada na tozo  kwa lengo la kutunisha mfuko wa Umwagiliaji.

Akizungumza mjini Iringa Bwana Kahongo amesema endapo wakulima katika Skimu za Umwagiliaji watachangia fedha za ada ya usajili na matunzo kwa wakati, itasaidia kuharakisha ukarabati wa Skimu zilizoharibika kutokana na athari zitokanazo na madhara ya mabadiliko ya tabia nchi pamoja na kujenga Skimu mpya nchini.




Ametolea mfano zoezi la kuurejesha mto Ruaha Mdogo katika njia yake ya asili limegharimu fedha kutoka mfuko wa Umwagiliaji ambao unahitaji kuwezeshwa na wakulima hao.

Kwa upande wake Bi Katarina Mlaga ambaye ni mkulima mkazi wa kijiji cha Magozi ameishukuru serikali kupitia Tume ya Taifa ya Umwagiliaji kwa kazi kubwa iliyofanya wa kurejesha mto Ruaha Mdogo katika njia yake ya asili, nakusema kuwa wakulima katika kijiji hicho hutegemea Zaidi kilimo cha umwagiliaji, na wamepata elimu ya kutosha kuhusu uchangiaji wa tozo za umwagiliaji na wapo tayari kuchangia.

Awali akiongea kijijini hapo Diwani wa kata ya Ilolo Mpya Bwana Funda  Mihayo   amemshukuru Mkurugenzi wa Tume ya taifa ya Umwagiliaji Bw, Daudi Kaali kwa kuwezesha wataalam wa tume kurekebisha miundombinu ya mifereji ya kupeleka maji katika mashamba ya wakulima pamoja na zoezi la usanifu linaloendelea katika Skimu ya Liganga ambapo lengo ni kuwezesha maji kunyweshea Skimu ya Magozi na  Mkombilenga.

Comments

Dodoma News
Mwanza City, Mwanza, Tanzania
Dennis G. Harrison, mmiliki mwenza wa Mtandao wa Dodoma News Blog, alizaliwa mkoani Morogoro zaidi ya miaka 40 iliyopita. Dennis ana Taaluma ya Uandishi wa Habari (Proffessional Journalism) kutoka Chuo Kikuu cha Mtakatifu Augustine (SAUT). Mwaka 2009 alimaliza Shahada ya Uzamili katika Mawasiliano ya Umma, ikijikita katika Menejimenti ya Uhusiano kwa Umma na Matangazo katika chuo cha SAUT. Mwaka 2002, Dennis aliajiriwa katika Shirika la Posta Tanzania, Ofisi kuu ya Mwanza. Mwaka 2009 aliajiriwa katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Iringa kwa nafasi ya Afisa Habari. Akiwa katika ofisi hiyo alifanya kazi kwa juhudu na maarifa na kufanikiwa kuchaguliwa na wafanyakazi wote kuwa mfanya kazi bora. Kufuatia juhudi na utendaji kazi wake, alipanda hadi nafasi ya Afisa Habari Mwandamizi.