TAASISI YA UTAFITI YATAKIWA KUISHIRIKISHA SERIKALI


Hafsa Omar-Dodoma

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Nishati, Kheri Mahimbali ameitaka Taasisi  inayojishughulisha na utafiti ya (Natural Resource Governance Institute) kuishirikisha Serikali kwenye tafiti zinazohusu Serikali ili kuwa na usahihi wa takwimu zinazotolewa.

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Nishati, Kheri Mahimbali akizungumza wakati wa kikao cha Wizara ya Nishati na Taasisi ya Natural Resource Governance Institute, kilichofanyika katika ofisi za Wizara ya Nishati, zilizopo katika mji wa Serikali, jijini Dodoma


Ameyasema hayo, Oktoba 29,2021 wakati wa kikao cha Wizara ya Nishati na Taasisi hiyo kilichofanyika katika ofisi za Wizara ya Nishati, zilizopo katika mji wa Serikali, jijini Dodoma ambapo  Taasisi hiyo iliwasilisha tafiti yao  kuhusiana na rasilimali ya Gesi Asilia nchini Tanzania.

Aidha, alisema ushirikiano wa Serikali na Taasisi hizo utasaidia kupata takwimu zilizo sahihi ambazo zitakuwa zenye manufaa kwa Taifa kiujumla.

“Haipendeza tafiti mbalimbali kusambazwa kwa wananchi bila ya Serikali kushirikishwa na kutoa maoni yao unapofanya tafiti lazima ungalie na upande wa pili ambao ni Serikali,” alisisitiza Mahimbali.

Alisema, Serikali itaendelea kufanya kazi na kushirikiana na Taasisi hiyo katika tafiti mbalimbali na kwakuwa inaisadia Serikali kupata takwimu mbalimbali muhimu.

Washiriki mbalimbali  kwenye kikao cha Wizara ya Nishati na Taasisi ya Natural Resource Governance Institute   kilichofanyika katika ofisi za Wizara ya Nishati, zilizopo katika mji wa Serikali


Kikao hicho, kilihudhiriwa na Kamishna Msaidizi wa Gesi, Mohamed FakihiKamishna Msaidizi wa Nishati Jadidifu, Edward IshegomaMkurugenzi wa Sera Mipango Petro Lyatuu pamoja  na watumishi mbalimbali wa Wizara ya Nishati na Taasisi zilizopo chini yake.

Comments

Dodoma News
Mwanza City, Mwanza, Tanzania
Dennis G. Harrison, mmiliki mwenza wa Mtandao wa Dodoma News Blog, alizaliwa mkoani Morogoro zaidi ya miaka 40 iliyopita. Dennis ana Taaluma ya Uandishi wa Habari (Proffessional Journalism) kutoka Chuo Kikuu cha Mtakatifu Augustine (SAUT). Mwaka 2009 alimaliza Shahada ya Uzamili katika Mawasiliano ya Umma, ikijikita katika Menejimenti ya Uhusiano kwa Umma na Matangazo katika chuo cha SAUT. Mwaka 2002, Dennis aliajiriwa katika Shirika la Posta Tanzania, Ofisi kuu ya Mwanza. Mwaka 2009 aliajiriwa katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Iringa kwa nafasi ya Afisa Habari. Akiwa katika ofisi hiyo alifanya kazi kwa juhudu na maarifa na kufanikiwa kuchaguliwa na wafanyakazi wote kuwa mfanya kazi bora. Kufuatia juhudi na utendaji kazi wake, alipanda hadi nafasi ya Afisa Habari Mwandamizi.