DODOMA.
Mbunge wa Viti Maalum Neema Lugangira ,amesema iko haja ya kupunguza msongamano wa wafungwa gerezani kwani idadi ya
mahabusu ni wengi kuliko wafungwa.
Lugangira ameyasema leo jijini Dodoma
katika wiki ya Asasi za kiraia iliyoanza tangu oktoba 23 na kutarajiwa
kuhimitimiswa leo oktoba 28 katika mdajadala wa haki ya dhamana kwenye makosa yasiyodhaminiwa.
Wakati huo Lugangira amesema , hivi sasa kuna
takribani mahabusu 17,000 huku wafungwa wakiwa ni 14,000. ‘’kwahiyo hapo
tunaona idadi ya mahabusu ni zaidi ya wafungwa’’
Mbali na hayo amesema kuwa njia pekee
ya kusaidia kupunguza idadi ya mahabusu ni kutoa dhamana kwa watu hao, kwani makosa ya mahabusu asilimia kubwa ni watu wenye makosa
yenye dhamana .
Hahivyo, Amesema mara zote anapoibua mijadala
ya namna hiyo ndani ya bunge amekuwa akipata ushirikiano ‘’Nadhani wengi mtakubalina nami, Mh. Rais Samia Suluhu
Hassan ameshasema mara kadhaa kuhusiana na suala la uchelewashaji wa kutoa
hukumu,msongamano mkubwa gerezani na hata mara ya mwisho alitoa maelekezo yake
kuwa angependa kuona tunapunguza msongamano mkubwa gerezani ‘’
Comments
Post a Comment