Na. Dennis Gondwe, Chinangali Park-DODOMA
JAMII imetakiwa kutoa kipaumbele kwa masuala ya ulinzi na usalama wa
mtoto ili kumuepusha na ukatili wa kijinsia na kumuhakikishia makuzi bora ili
aweze kuwa raia mwema na kutoa mchango wake kwa taifa.
| Afisa Utawi wa Jamii katika Jiji la Dodoma, Heriely Kutwama akitoa elimu kwa kundi la watoto waliotembelea banda la Idara ya Afya |
Kauli hiyo ilitolewa na Afisa Ustawi wa Jamii katika Halmashauri ya Jiji
la Dodoma, Rebeka Ndaki alipokuwa akielezea umuhimu wa ulinzi na usalam wa
mtoto katika jamii kwa wananchi
waliotembelea banda la Idara ya Afya la Halmashauri hiyo katika Bustani ya Mapumziko
Chinangali jijini Dodoma kwenye maonesho ya Karibu Dodoma Festival.
Ndaki alisema kuwa watoto wote wana haki ya kuishi katika mazingira bora
na salama yasiyo na aina yoyote ya vitendo vya ukatili. “Kila mtoto ana haki ya
kuishi na kufuraia maisha yake katika jamii kama walivyo watoto wengine. Na mwenye
jukumu la kumhakikishia mtoto ulinzi na usalama wake ni jamii nzima
inayomzunguka mtoto” alisema Ndaki.
Afisa Ustawi huyo alisema kuwa watoto wamekuwa wakifanyiwa vitendo vya
kikatili sana katika jamii. Bahati mbaya jamii nayo imekuwa ni sehemu ya kuuendeleza
ukatili huo. Vitendo vivyo vimekuwa vikiwaathiri Watoto kisaikolojia na
kimakuzi na kuzuia kutimizwa kwa ndoto zao, alisema. “Nitumie nafasi ya
maonesho haya ya Karibu Dodoma Festival kuikumbusha jamii kuwa ndiyo mlinzi
namba moja wa mtoto. Sisi kama Halmashauri tumeshiriki katika maonesho haya
kutoa elimu kwa wananchi juu ya umuhimu ulinzi na usalama wa mtoto dhidi ya
vitendi vya kikatili. Lakini pia tupo hapa kuelezea huduma zinazotolewa na Seksheni
ya Ustawi wa Jamii iliyo chini ya Idara ya Afya katika Halmashauri ya Jiji la
Dodoma” alisema Ndaki.
Aidha, alizitaja huduma zitolewazo na seksheni hiyo kuwa ni elimu ya usajili ya vituo vya kulelea watoto wadogo mchana ‘day care’, elimu ya ukatili
wa kijinsia na Watoto na huduma ya familia na
malezi. Huduma nyingine alizitaja kuwa ni usajili wa vyeti vya kuzaliwa kwa watoto wenye umri chini ya miaka 5 na
huduma ya msaada wa kisaikolojia.
MWISHO
Comments
Post a Comment