WANAWAKE CHAMA CHA WAFANYAKAZI TUGHE WAPONGEZWA

 Na Rhoda Simba, Dodoma.

MWENYEKITI wa Chama cha Wafanyakazi wa Serikali kuu na Afya TUGHE Taifa , Archie Mmtambo amesema wanawake ndio wamekisimamisha Imara chama hicho kwani huko nyuma chama kilionekana kulegalega.


Kadhalika amewataka wafanyakazi kuacha kuogopa kujiunga na chama hicho kwani lengo kuu la kuanzishwa kwa TUGHE ni kutetea maslahi ya wafanyakazi na si chama cha kiharakati kama ilivyo kuwa ikisemwa hapo awali.

Ameyasema hayo leo September 28 jijini hapa wakati akifungua Mkutano Mkuu wa uchaguzi wa wanawake TUGHE ambapo ameeleza kuwa lengo kuu la mkutano huo ni kufanya uchaguzi wa viongozi kwa nafasi mbalimbali wa chama hicho kwa upande wa wanawake .

"Mpaka kufikia hapa TUGHE imesimamishwa na wanawake, huko nyuma chama kiliyumba sana na yale maneno ya kwamba kujiunga na chama ni kama uanaharakati wa kupinga yale yanayosemwa na waajiri wetu  lakini tunawashuru kina mama hawa ndio waliosababisha Chama hiki kusimama" amesema Mmtambo.

Kwa upande wake Katibu wa TUGHE Hery Mkunda ambaye amemaliza muda wake na anawania nafasi hiyo kwa mara nyingine tena amesema mkutano huo unafanyika kila baada ya miaka mitano ambapo wanawake  wa chama hicho huchagua viongozi wa nafasi mbalimbali.

"Leo ni uchaguzi wa TUGHE  wanawake lakini ikumbukwe kwamba katika katiba yetu ya TUGHE imeainisha kutoa  kipaumbele kwa makundi maalumu ikiwemo wanawake walemavu na vijana," 

Na kuongeza kuwa "Wanawake wamepewa kipaumbele zaidi kwani huko nyuma hawakuwa wakipata au kupewa nafasi sasa tumewaona wanawake na tunawapa nafasi ili waweze kujitegemea wenyewe na waimarishe chama,"  amesema Mkunda

Hata hivyo TUGHE Taifa inatarajia kufanya uchaguzi wa viongozi hapo kesho September 29 utakaojumuisha mwenyekiti Taifa Katibu sambamba na wajumbe mbalimbali.

 

 

Comments

Dodoma News
Mwanza City, Mwanza, Tanzania
Dennis G. Harrison, mmiliki mwenza wa Mtandao wa Dodoma News Blog, alizaliwa mkoani Morogoro zaidi ya miaka 40 iliyopita. Dennis ana Taaluma ya Uandishi wa Habari (Proffessional Journalism) kutoka Chuo Kikuu cha Mtakatifu Augustine (SAUT). Mwaka 2009 alimaliza Shahada ya Uzamili katika Mawasiliano ya Umma, ikijikita katika Menejimenti ya Uhusiano kwa Umma na Matangazo katika chuo cha SAUT. Mwaka 2002, Dennis aliajiriwa katika Shirika la Posta Tanzania, Ofisi kuu ya Mwanza. Mwaka 2009 aliajiriwa katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Iringa kwa nafasi ya Afisa Habari. Akiwa katika ofisi hiyo alifanya kazi kwa juhudu na maarifa na kufanikiwa kuchaguliwa na wafanyakazi wote kuwa mfanya kazi bora. Kufuatia juhudi na utendaji kazi wake, alipanda hadi nafasi ya Afisa Habari Mwandamizi.