DODOMA.
Imeelezwa kuwa vyanzo vya msongo wa mawazo vinatokana na aina ya wingi wa kazi anazozifanya mtu
hasa akiwa anafanya kazi ngumu au wakati mwingine kazi hiyo iwe na maslahi
kidogo.
Vyanzo vingine vikiwa ni Mila na Desturi kinzani zinazo
sababisha maumivu ya hisia, ubaguzi, kudhalilishwa na kuonewa.
Kauli hiyo imetolewa na Sylivia Siriwa katibu Mtendaji Mkuu wa Asasi ya Saiko
Senta iliyopo jijini Dodoma wakati akizungumza na Mtandao wa Dodoma News Blog ofisini kwake kuhusiana na mada ya msongo wa mawazo , amesema wakati mwingine kushindwa kutoa maamuzi sahihi
ambayo ni bora na kwa wakati hiyo nayo inatokana msongo wa mawazo.
‘’lakini kukosa uthubutu wa kukabiliana na changamoto yaani
ujasiri nakujiamini ,hii inawapata watu wengi wanaoishi kwa hofu, wasiwasi
anashindwa, anakosa uthubutu wa kukabiliana na changamoto’’ amesema
Ameongeza kuwa Kupata matukio ya kuumiza nafsi mfululizo ametaja kuwa chanzo cha msongo wa mawazo ambayo huwa ni magumu kuyapokea.
‘’
kama vile kufiwa na wapenzi, kuachana, kufukuzwa kazi, kushindwa masomo na vitu
vinavyofanana kama hivyo ambavyo vinaleta matokeo hasi’’
Katika hatua nyingine Sylivia amesema kuna na madeni makubwa na yenye riba ambayo familia ikishindwa kulipa hupelekea msongo wa mawazo .
''kufanya
kazi bila ratiba kamili nayo inapelekea msongo wa mawazo, kukatishwa tamaa kila
mara hata uanapofanya kila jitihada wenzako wanakukatisha tamaa ni chanzo cha
msongo wa mawazo pamoja na ulaji usio faa sasa hivi kuna vyakula ambazo vinaliwa baadaye
vinasabisha matatizo ya kiafya navyo vinasabisha msongo wa mawazo''
Hatahivyo, ameshauri watu kuishi maisha yenye hisia chanya na kuachana na ile dhana ya kumuona kila mtu ana
makosa hali hiyo itasaidia kuondokana na
changamoto za msongo wa mawazo.
Mwisho.
Comments
Post a Comment