VIJIJI 134 WILAYANI IRINGA VYAFIKIWA NA ELIMU YA UVIKO-19



Na. WAMJW-Iringa

Wilaya ya Iringa wameweza kuvifikia vijiji  vyote 134 vilivyopo kwenye wilaya hiyo kwa kutoa elimu na uhamasishaji wananchi kuelewa umuhimu wa chanjo  dhidi ya UVIKO-19  na kusababisha muitikio mkubwa wa uhitaji wa chanjo hiyo.

Akiongea na Kaimu Mkuu wa Kitengo cha habari Serikalini kutoka Wizara ya Afya ,Mratibu wa huduma za chanjo wilaya ya Iringa Bw. Sospeter Tiara amesema wananchi katika vijiji hivyo vyote wamekua na mwitikio mkubwa kiasi kwamba imefikia hatua baadhi ya zahanati na maeneo yao kuishiwa chanjo hiyo na hivyo kuweza kuchukua kwenye vituo vingine.

Tiara amesema wameweza kufikia hatua hiyo kwa kuwa kabla ya kuanza kwa utekelezaji wa Mpango wa Jamii Shirikishi na Harakishi dhidi ya UVIKO-19 unaporatibiwa na Wizara ya Afya na TAMISEMI wao kama wilaya waliweza kutoa elimu  kwenye vijiji hivyo hali iliyopelekea wananchi wengi kuelewa na kuondoa hofu dhidi ya chanjo hiyo.

“Awali wananchi wengi walikua wanaogopa chanjo na wengi walikuwa na  maswali mengi juu ya chanjo hii na hivyo kutokuwa na mwitikio mkubwa, lakini mpaka sasa baada ya kuanza kwa mpango huu tumeweza kutoa elimu na kuwafikia wananchi mahali walipo ikiwemo  nyumba za ibada na maeneo yao ”.

Kwa upande wa wanawake Tiara amesema  kuwa kutokana kutoa elimu ya kutosha kwa wananchi hivi sasa wanawake wameweza kujitokeza kwa wingi tofauti na awali ambapo wanawake waliamini chanjo hiyo inazuia uzazi“baada ya kuwahamasisha na kuwapatia elimu na kuwathibitishia chanjo hii ni salama , pia waliona watoa huduma wetu wakipata chanjo hii waliamini na kuweza kujitokeza “.Alisema

Naye, Mganga Mfawidhi wa kituo cha afya Kimande  Salim Salim amesema wameweza kushirikiana na Serikali ya kijiji cha Itunundu katika utoaji wa elimu kwenye nyumba za ibada,majumbani n ahata maeneo yenye mikusanyiko na hivyo kuongeza hali ya hamasa kwa wananchi.

“Pia tunamshukuru Mbunge wetu Mhe. William Lukuvi,Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo na Makazi kwa kufika kwenye kata hiyo na kuwahamasisha wananchi wa kata ya  ya Itunundu kwa kuwathibitishia chanjo hiyo ni salama”.

Awali Mratibu wa huduma ya mama na mtoto Bi. Leonida kalinga Mratibuamesema kuwa hivi sasa akina mama wamekua wameanza kuelewa kwani hapo awali walikua hawajui maana ya chanjo na hivyo wanap[ofuika kwenye kliniki ya mama na mtoto wanawapatia elimu na kuweza kupata chanjo hiyo na kuongeza kuwa akina mama wamekua wakiuliza maswali mengi na baada ya elimu wanajitokeza kuchanja.

Mwasho.


Comments

Dodoma News
Mwanza City, Mwanza, Tanzania
Dennis G. Harrison, mmiliki mwenza wa Mtandao wa Dodoma News Blog, alizaliwa mkoani Morogoro zaidi ya miaka 40 iliyopita. Dennis ana Taaluma ya Uandishi wa Habari (Proffessional Journalism) kutoka Chuo Kikuu cha Mtakatifu Augustine (SAUT). Mwaka 2009 alimaliza Shahada ya Uzamili katika Mawasiliano ya Umma, ikijikita katika Menejimenti ya Uhusiano kwa Umma na Matangazo katika chuo cha SAUT. Mwaka 2002, Dennis aliajiriwa katika Shirika la Posta Tanzania, Ofisi kuu ya Mwanza. Mwaka 2009 aliajiriwa katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Iringa kwa nafasi ya Afisa Habari. Akiwa katika ofisi hiyo alifanya kazi kwa juhudu na maarifa na kufanikiwa kuchaguliwa na wafanyakazi wote kuwa mfanya kazi bora. Kufuatia juhudi na utendaji kazi wake, alipanda hadi nafasi ya Afisa Habari Mwandamizi.