Tanzania itaendelea kushirikiana
na nchi Jumuiya za Umoja wa Afrika ili kuendeleza utalii kwa lengo la kukuza
uchumi wa nchi wanachama.
Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Mary Masanja (Mb)
katika Maadhimisho ya Siku ya Utalii Duniani 2021 yaliyofanyika Jijini Abidjan
nchini Côte d' Ivoire leo.
“Lengo kuu la kushiriki katika Maadhimisho haya ni kujifunza na kuangalia
namna ya kendeleza utalii wetu hasa katika kipindi hiki cha kukabiliana na
janga Uviko 19 lililoikumba dunia”amesisitiza Mhe. Masanja.
Aidha, Mhe. Mary Masanja ameongeza kuwa ushiriki huo ni fursa ya kubadilishana
uzoefu na pia kuvitangaza vivutio vya Utalii vilivyoko nchini Tanzania ikiwa ni
moja ya juhudi za kuunga mkono kazi anayoifanya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan ya kutangaza utalii duniani.
Kauli mbiu ya Siku ya Utalii Duniani kwa mwaka huu ni “Utalii kwa Maendeleo
Shirikishi/ Jumuishi”

Comments
Post a Comment