RAIS SAMIA AHIMIZA USIMAMIAJI WA MIRADI YA MAENDELEO

 


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ,Samia Suluhu Hassan ameagiza Mamlaka za Serikali za Mitaa kusimamia miradi ya maendeleo ili kuendana na thamani halisi ya kushirikisha wananchi kwenye miradi kwani mamlaka hizo   ni nguzo na kiungo muhimu kati ya wananchi na serikali. 

Rais Samia amesema hayo leo Septemba 27,2021 jijini Dodoma  katika Mkutano  Mkuu  Maalum wa Uchaguzi wa Jumuiya ya Mamlaka za Tawala Serikali za Mitaa Tanzania ALAT.

Wakati huo huo, Rais Samia ameagiza  kutumia mitandao Zaidi katika ukusanyaji wa mapato na utatuzi wa migogoro ya ardhi na kutekeleza miradi ya maendeleo kwa thamani halisi na kusimamia vyema fungu la asilimia 10 kwa ajili ya mikopo.

Kuhusu suala la ushirikishwaji wa wananchi kwenye miradi ya maendeleo, Rais Samia amesema ni jambo la msingi kwa ajili ya maendeleo huku akiahidi kujenga madarasa 15,000 kote nchini  hivyo mwezi januari hakutakuwa na migawanyo ya awamu kuripoti  shuleni kwa kigezo cha kukosa vyumba vya madarasa.

Katika  kero mbalimbali kwa wananchi ikiwemo migogoro ya miradhi na migogoro ya ardhi ,Rais Samia amewataka viongozi serikali za mitaa kutenda haki na kuacha mivutano kwa viongozi serikali za mitaa ikiwemo madiwani,wakurugenzi na wakuu wa wilaya kwani mivutano iliyo mingi ipo kwa  maslahi binafsi.

Kwa upande wake Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kassim Majaliwa ,amesema kupitia mfumo wa Force Account kumekuwa na uaminifu mkubwa katika halmashauri kwenye utekelezaji miradi ya maendeleo.

Naye Spika wa Bunge la Jamhuri wa Muungano wa Tanzania Job Ndugai amesema suala la utengaji wa fedha za maendeleo kwa kila halmashauri ni muhimu kwa mujibu wa kanuni  na taratibu ambapo kwa upande wa halmashauri ni asilimia 40 na manispaa  na majiji kwa asilimia 60.

Waziri wa Nchi ,Ofisi ya Rais,Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa TAMISEMI Ummy Mwalimu amesema maamuzi ya serikali kuanza kulipa posho madiwani limepokelewa vyema kwani imerudisha hadhi na heshima huku akiwataka viongozi wote kusimamia vyema miradi ya maendeleo  ambapo hadi sasa halmashauri zimeshapokea  Tsh.bilioni  298 kwa ajili ya miradi mbalimbali ya maendeleo.

Mkutano  Mkuu  Maalum wa ALAT unakwenda  sambamba na kauli mbiu isemayo ”Chagua viongozi bora  kwa maendeleo endelevu “ambapo uchaguzi wa ALAT unaongozwa na kanuni za kudumu  ukihusishwa na wajumbe mbalimbali ikiwemo Mayeya wa majiji na manispaa na wakurugenzi wa halmashauri kote nchini.

 

MWISHO.

 

Comments

Dodoma News
Mwanza City, Mwanza, Tanzania
Dennis G. Harrison, mmiliki mwenza wa Mtandao wa Dodoma News Blog, alizaliwa mkoani Morogoro zaidi ya miaka 40 iliyopita. Dennis ana Taaluma ya Uandishi wa Habari (Proffessional Journalism) kutoka Chuo Kikuu cha Mtakatifu Augustine (SAUT). Mwaka 2009 alimaliza Shahada ya Uzamili katika Mawasiliano ya Umma, ikijikita katika Menejimenti ya Uhusiano kwa Umma na Matangazo katika chuo cha SAUT. Mwaka 2002, Dennis aliajiriwa katika Shirika la Posta Tanzania, Ofisi kuu ya Mwanza. Mwaka 2009 aliajiriwa katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Iringa kwa nafasi ya Afisa Habari. Akiwa katika ofisi hiyo alifanya kazi kwa juhudu na maarifa na kufanikiwa kuchaguliwa na wafanyakazi wote kuwa mfanya kazi bora. Kufuatia juhudi na utendaji kazi wake, alipanda hadi nafasi ya Afisa Habari Mwandamizi.